Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
CHANJO
dhidi ya virusi vya Corona (Covid-19) iliyochakatwa katika Chuo kikuu
cha Oxford nchini Uingereza itafanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza siku
ya Alhamisi wiki hii, katibu wa Afya nchini humo Matt Hancock ameeleza.
Kwa mujibu wa DailyMail imeelezwa kuwa Hancock amesema kuwa chanjo itakua ni njia sahihi ya Kupambana na virusi hivyo.
Chanjo
hiyo itafanyiwa majaribio kwa watu wapatao 510 wenye umri kati ya miaka
18 hadi 55 huku ikielezwa kuwa watafiti hao wanaimani ya kuwapa watu
ulinzi dhidi ya Covid -19.
Aidha
imeelezwa kuwa Serikali nchini humo itatoa fedha za ziada zipatazo Euro
milioni 20 kwa wanasayansi kutoka ili kuwezesha majaribio yao pamoja na
Euro milioni 22.5 kwa chuo cha Imperial London.
Chanjo
hiyo iliyochakatwa na chuo kikuu cha Oxford inajulikana kwa jina la
ChAdOx1 nCoV-19 na itafanyiwa majaribio kwa watu 510 kutoka makundi
1,112 wenye umri kati ya miaka 18 hadi 55 ambao walijitolea kutoka
London, Bristol, Oxford na Southampton.
Imeelezwa
kuwa Uingereza inakua nchi ya kwanza kutengeneza na kufanya majaribio
ya chanjo hiyo Jambo ambalo linaleta matumaini ya watu kutoka katika
karantini na kuidhibiti Covid -19.
Pia
Hancock amesema kuwa licha ya ugonjwa huo kuwa mpya kila jitihada
zitafanyika ambapo hadi sasa wanasayansi kutoka Oxford na Imperial
wameongoza katika zoezi hilo na Serikali itafanya kila liwezekanalo
katika kushiriki na kufanikisha hilo.
Hadi
Sasa watu walioathirika na virusi hivyo nchini Uingereza imefikia
125,000 pamoja na vifo 17,339 jambo ambalo limewasukuma Uingereza
kupambana janga hilo ambalo linatikisa dunia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...