Na Said Mwishehe,Michuzi TV

TAHARUKI kubwa imeibuka leo katika Hospital ya Amana jijini Dar es Salaam baada ya baadhi ya wagonjwa wa  Covid-19 waliokuwa wanapatiwa matibababu kufanya vurugu na kutaka kuondoka warudi majumbani kwao.

 Taarifa za wagonjwa wa Covid-19 kufanya vurugu za kutaka kuondoka Hospitali ya Amana zilianza kusambaa Kama upepo tangu asubuhi ya leo, hata hivyo inaelezwa  walinzi waliokuwa hospitalini hapo kutoka Suma JKT wamefanya kazi kubwa ya kutuliza vurugu zilizoanzishwa na wagonjwa hao.

Kwa mujibu wa wagonjwa hao walikuwa na hoja mbili ,moja wanadai tangu wafike Hospitali ya  Amana huduma za dawa ni hafifu na hoja ya pili wanadai  huduma ya chakula ni duni kiasi wanahisi wanaweza kufa kwa njaa badala ya Corona.

 Hata hivyo mmoja wa wagonjwa wa Covid-19 waliokuwepo kwenye maandamano hayo( jina limehifadhiwa)  amesema kuwa kwanza ifahamike hawakutoroka bali waliamua kutumia ujasiri kufikisha ujumbe wao kwa Serikali na Umma ujue na hasa ha huduma duni.

"Hakuna aliyetoroka ,ila tuliamua kufikisha ujumbe Wetu, tulitoka wodini na kwenda geti la nje kutoa malalamiko yetu maana tulitaka Umma ujue kinachoendelea kwa wagonjwa wa Corona.Huduma zimekuwa hafifu na hakuna anayejali.Hivyo tumepaza sauti zetu na baada ya hapo angalau wamekuja kufanya usafiri wodini.

" Tunatambua kutoroka hospitalini maana yake tunapeleka ugonjwa majumbani na hatuko tayari kufanya hivyo.Tumebaki ili tuendelee na matibabu kwani wapo ambao wamechukuliwa vipimo kwa mara ya kwanza na wengine mara ya pili," amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Dk.Sophia Mjema amekiri kulikuwepo kwa taharuki hiyo na kwamba amesema madai ya kwamba kuna wagonjwa wametoroka atafuatilia lakini akatoa rai kwa wagonjwa hao kuendelea kubaki hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Amesema  na iwapo kuna wagonjwa wanatakiwa kutoka basi watatoka kwa utaratibu  wa watoa huduma za afya na si vinginevyo." Tunaomba wagonjwa waendelee kutulia wakati madaktari wakiendelea kuwapatia matibabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...