Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (kulia) akiteta jambo na Msajili
Msaidizi wa Vyama vya Siasa (ARPP), Sisty Nyahoza wakati wa zoezi la
uhakiki wa uhai wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu katika Ofisi
ya Makao Mkuu ya Chama hicho jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akielezea jambo mbele ya ugeni kutoka
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) walipomtembelea ofisini kwake
wakati wa zoezi la uhakiki wa uhai wa vyama vya siasa vyenye usajili wa
kudumu katika Ofisi ya Makao Mkuu ya Chama hicho jijini Dodoma leo.
Kutoka kushoto ni Katibu wa NEC – Oganaizesheni wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), Ndg. Pereira Ami Silima, Mkuu wa Kitengo cha Usajili wa Vyama vya
Siasa, Muhidin Mapeyo na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty
Nyahoza.
Katibu wa NEC –Idara ya
Oganaizesheni ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Pereila Ami Silima
akizungumza wakati wa zoezi la uhakiki wa uhai wa vyama vya siasa vyenye
usajili wa kudumu katika Ofisi ya Makao Mkuu ya chama hicho jijini
Dodoma leo. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) imeendesha zoezi
la uhakiki ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa kukagua uhai wa vyama vya
siasa nchini.
Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya
Oganaizesheni ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwangi Rajab Kundya akitoa
maelezo wakati wa zoezi la uhakiki wa uhai wa vyama vya siasa vyenye
usajili wa kudumu katika Ofisi ya Makao Mkuu ya chama hicho jijini
Dodoma leo. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) imeendesha zoezi
la uhakiki ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa kukagua uhai wa vyama vya
siasa nchini.
Kutoka kushoto ni Msajili Msaidizi
wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza,Mkuu wa Kitengo cha Usajili wa Vyama
vya Siasa, Muhidin Mapeyo na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Elimu ya Uraia toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), Abuu
Kimario wakikagua baadhi ya nyaraka za usajili wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) wakati wa zoezi la uhakiki wa uhai wa vyama vya siasa siasa vyenye
usajili wa kudumu katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho leo jijini
Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa
Chama cha Mapinduzi (CCM), Goodluck Mwangomango akifafanua jambo mbele
ya ujumbe kutoka Ofisi ya Masjili wa Vyama vya Siasa (ORPP) wakati wa
zoezi la uhakiki wa uhai wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu
katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho leo jijini Dodoma.Kushoto ni
Afisa Tehama wa CCM, Magoti Marwa na kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu –
Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Christopher
Magala.
Katibu Msaidi Mkuu – Idara ya
Uchumi na Fedha, Victor Septemba Patrick akifafanua jambo mbele ya
ujumbe kutoka Ofisi ya Masjili wa Vyama vya Siasa (ORPP) wakati wa zoezi
la uhakiki wa uhai wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu katika
ofisi za Makao Makuu ya chama hicho leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akionyesha hati za usajili na bodi ya
wadhamini za CCM wakati wa zoezi la uhakiki wa uhai wa vyama vya siasa
vyenye usajili wa kudumu katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho leo
jijini Dodoma. Kanuni za Sheria ya Usajili wa Vyama vya Siasa ya Mwaka
2019 inataka hati hizo kutundikwa ukutani katika ofisi za vyama hivyo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akielezea jambo wajumbe kutoka Ofisi
ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) MARA mara baada ya kumaliza zoezi
la uhakiki wa uhai wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu katika
ofisi za Makao Makuu ya chama hicho leo jijini Dodoma.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya
Siasa (ARPP), Sisty Nyahoza akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mstaafu wa
Awamu ya Nne na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mhe. Mizengo Pinda
walipokutana katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma leo
walipofika katika ofisi hizo kwa ajili ya zoezi la uhakiki wa uhai wa
vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu katika ofisi za Makao Makuu ya
chama hicho leo jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...