NA MWANDISHI WETU.

MKUU wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera amewataka Wazazi na Walezi kuwa kitu kimoja kwa wakati huu nchi na Dunia kwa ujumla zipo kwenye mapambano ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19).

Ambapo amewataka kuwa karibu na familia zao kwa sasa na kuacha mifarakano ambayo itawatenganisha.

DC Tano Mwera ametoa rai hiyo leo 15 Mei ambapo Dunia inaadhimisha siku ya Familia Duniani."Wana Busega ni familia moja tuendelee kushirikiana na kuchukua hatua dhidi ya Corona.

Wazazi na Walezi nyie ndio mpo na hizi familia huko majumbani tuimalishe umoja na tuchukue tahadhari zaidi". Alisema DC Tano Mwera.

Pia amewataka wazazi kutotumia watoto kwenye shughuli za kujipatia mali ama kipato ikiwemo kuwatumikisha mashambani na baadala yake wawahimize kujisomea na kuwalea kwenye misingi ya maadili.

"Tuhakikishe watoto wanajengewa misingi bora. Tuwapangie muda wa kujisomea na kusaidia kazi za nyumbani. Marufuku kutuma watoto kwenye mashamba ama machimbo kwa lengo la kujipatia kipato mzazi ama mlezi atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria" alisema DC Tano Mwera.

Aidha, DC Tano Mwera amewataka Wananchi wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanawalinda Wazee ikiwemo kulinda haki zao za msingi kama matibabu na lishe kutoka kwa watu wao wa karibu kwani Wazee hao awali walijenga misingi walioikuta sasa.

Katika kukabiliana na janga la Corona pia amewataka Wananchi wa Busega kufuata maelekezo na ushauri wa wataalamu wa afya wa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, kuwa na utaratibu wa kunawa mikono kwa maji tiririka mara kwa mara na kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko ya watu.

kila tarehe 15 mwezi Mei ni siku ya Familia Duniani ambayo kwa Mwaka huu inaongozwa na Kauli Mbiu "Familia ni Msingi katika kutokomeza Corona, tuilinde na tuwalinde wengine".

Wilaya ya Busega ni miongoni mwa Wilaya za Mkoa wa Simiyu.


Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...