Na Mwandishi Wet u,Michuzi TV

KAIMU Msajili Bodi Ya Nyama Tanzania Iman Sichalwe amefanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha nyama cha Tanchoice Soga kibaha mkoani Pwani.

Kiwanda hicho ni kikubwa Afrika Mashariki na Kati kwenye Sekta ya mifugo na kutajwa kuwa mkombozi mkubwa kwa wadau wa sekta ya nyama Nchini Ambapo kitakuwa na uwezo wa kuchinja ng'ombe 1000 na mbuzi 4500 kwa siku.

Akiwa kiwandani haoo baada ya kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho, Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania Sichalwe amesema amejiridhisha kuwa kimekamilika kwa asilimia 99 na kilichobaki ni hatua za mwisho kabisa kuanza kufanya Kazi na kuwataka Wafugaji kukaa mkao wa Kula.

Aidha amesema uwekezaji wa kiwanda hicho ni mkubwa kwenye Sekta ya mifugo ambao unatajwa kuleta matokeo chanya katika uchumi wa nchi.

Pia amewataka wafugaji kufuga kisasa na kuachana na kufuga kwa mazoea na kama bodi wenye dhamana kubwa ya uusimamia,kuendeleza na kuratibu sekta ya nyama nchini wataendelea kutoa elimu ya umuhimu wa uongezaji dhamani ya mazao ya mifugo na kutambua namna bora ya kunenepesha mifugo ili kupata nafasi ya kuuza mifugo yao kwenye kiwanda hicho.
 Muonekano wa ndani wa Ujenzi wa kiwanda hicho cha Nyama  cha Tanchoice ikiwemo mashine za kisasa za kukatia Nyama.

 Hapa kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Bwana Iman Sichalwe(watatu toka kulia) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Rashid Abdullah wa kwanza toka kulia akitoka kukagua magari maalumu yatakayo tumika kubebea nyama kutoka kiwandani hapo Soga Kibaha mkoani Pwani kuelekea Airport tayari kusafirishwa nje ya nchi.
  Muonekano wa nje wa kiwanda hicho cha nyama
 Kaimu Msajili wa Bodi Ya Nyama Nchini Tanzania Bwana Imani Sichalwe alievaa Suti ya blue akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Tanchoice Soga wilayani Kibaha mkoani Pwani.
 Kaimu Msajili Bodi ya Nyama Tanzania  Imani Sichalwe( mwenye suti ya blue)akitoka kukagua maabara ya Kiwanda hicho.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...