MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa mashahidi 33 wanatarajiwa kuwepo katika kesi ya mauaji ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi inayowakabili washtakiwa sita pamoja na na vielelezo 18 .

Washtakiwa katika kesi hiyo ambao leo Mei 11,  2020 wamesomewa maelezo ya mashahidi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upelelezi kukamilika ni Msigwa Matonya, Mianda Mlewa, Paulo Mdonondo, Juma Kangungu, Longishu Losingo na John Mayunga.

Akisoma maelezo hayo Wakili wa Serikali, Anna Chimpaye amedai kuwa upande wa mashtaka utakuwa na jumla ya mashshidi 33 na vielelezo 18 wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Chimpaye alivitaja miongoni mwa vielelezo hivyo ni cheti cha kifo, ripoti kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na ramani ya tukio huku akiwataja baadhi ya mashahidi kuwa Ally Abdalah mjumbe wa shina namba 33 wa eneo la Kiwalani Migombani

Akisoma maelezo ya shahidi huyo amedai Novemba 12, 2013 akiwa nyumbani kwake walifika watu watano wakitaka kufanya upekuzi katika nyumba ya Mayunge maarufu kama Ngosha ambapo katika upekuzi huo walikuta Bastola ndogo aina ya Revolva, risasi 21 na baruti nne zilizokuwa ndani ya mfuko wa Plastiki zilizofichwa ndani ya nyumba hiyo juu ya paa la nyumba pembeni.

Hakimu Huruma Shahidi alisema kesi hiyo imehamishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kusikilizwa hivyo taarifa ya kuanza kusikilizwa itatolewa baada ya kupangwa.

Katika kesi ya msingi washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kuwa Novemba 3 mwaka 2013 huko Mbezi Msakuzi Kiswegere walimuua kwa kukusudia Dk.Sengondo Mvungi .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...