Mnamo tarehe 30/04/2020 tulichapisha habari  kuhusu sakata la wafanyakazi wa Impala Group na Hoteli ya Naura iliyopo Arusha ambapo mwakilishi wetu huko alileta habari kwamba alimhoji Ndugu Siya Lyimo, jambo ambalo imeonekana siyo kweli na kuleta usumbufu kwa Ndugu Sia Lyimo na kuhatarisha kumchonganisha na viongozi wa mkoa na wilaya ya Arusha.

Tunaomba radhi kwa ndugu Sia Lyimo kwa taarifa hiyo ambayo tunakukiri kwamba inaonesha hakuwahi kuhojiwa na mwakilishi wetu huyo; na ambaye kwa kosa hilo tunamchukulia hatua kali kwani ni kinyume cha maadili ya taaluma na weledi wa tasnia ya habari na pia kwa Blog inayoheshimika kama hii.

UONGOZI
MICHUZI BLOG

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...