Na Magreth Kinabo –Mahakama .
Agizo hilo lilitolewa na Prof. Juma kupitia mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Mwanza, la kuongeza matumizi ya TEHAMA kwenye kipindi hichi ambacho Tanzania na dunia kwa ujumla kukumbwa na janga la ugonjwa huo.
Mahakama
ya Tanzania imefanikiwa kuendesha mashauri 4,711 kwa njia ya Mahakama
Mtandao maarufu kama ‘Video Conference’ ikiwa ni hatua mojawapo za
kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa
COVID 1 9 katika kipindi cha miezi miwili.
Mashauri hayo
yamesikilizwa kwa njia hiyo, kufuatia utekelezaji wa agizo la Jaji
Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma alilolitoa Machi 23, mwaka
huu la kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili
kuwaepusha Watumishi wa Mahakama, Magereza, wafungwa na mahabusu na
wateja wengine wa Mahakama dhidi ya maambukizo hayo, wakati shughuli za
utoaji haki zikiendelea kufanyika.
Agizo hilo lilitolewa na Prof. Juma kupitia mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Mwanza, la kuongeza matumizi ya TEHAMA kwenye kipindi hichi ambacho Tanzania na dunia kwa ujumla kukumbwa na janga la ugonjwa huo.
Akizungumzia
kuhusu usikilizaji wa mashauri kwa kutumia teknolojia hiyo, Mkurugenzi
Msaidizi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Bw. Machumu
Essaba alisema imelipunguzia pia Jeshi la Magereza gharama za usafiri
wa kila siku za kuwaleta wafungwa au mahabusu mahakamani na msongamano.
‘‘Njia
hii imetumika katika kipindi cha ugonjwa huu, kuanzia Machi 23, mwaka
huu hadi Mei 26, mwaka huu, ambapo Mahakama ya Rufani Tanzania,
imesikiliza mashauri 48 kupitia vikao vitano, kati ya hivyo vitatu
vilifanyika katika Jiji la Dar es Salaam, vilivyohusisha mashauri 30 na
kimoja Tabora kilichohusisha mashauri tisa na kingine Iringa kilichokuwa
na mashauri tisa,’’ alisema Essaba.
Alisema kuwa
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imesikiliza mashauri
3,188 kati ya hayo, mashauri 804 ymesikilizwa na Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Mahakama za Wilaya, Kinondoni 714, Ilala 992, Temeke 523,
na Kigamboni 155.
Mahakama
Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya, Mahakama ya Mkoa na Wilaya mashauri
yaliyosikilizwa kwa teknolojia hiyo ni 367, kanda zingine ni Tanga
310, Musoma 158, Tabora 130, Dodoma 78, Mtwara 66, Moshi 46, Arusha 41,
Kigoma, 37, Sumbawanga 23, Iringa 15, Songea 14, Shinyanga 12, Mwanza
28 na Bukoba 5.
Essaba alifafanua
kwamba Mahakama Kuu Divisheni za Biashara imesikiliza mashauri 55 na
Kazi mashauri 90, ambazo zilitumia vifaa vilivyopo kwenye maeneo yao.
Aidha aliongeza
kwamba zaidi mashauri 300 yamesikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania
Kanda ya Mwanza kwa kutumia simu ya mezani ‘Teleconference’ kwa sababu
kuna tatizo la ukosefu wa huduma ya mtandao ‘internet’ kwenye ofisi za
Mwanasheria wa Serikali, hali inayosababisha kutumia njia hiyo.
Uongozi
wa Mahakama katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kukabiliana na
Virusi vya Corona ulikabidhi vifaa vya TEHAMA kwa Maafisa TEHAMA wa
kanda 16 za Mahakama Kuu yaTanzania Aprili 16 mwaka huu ili kuziwezesha
Mahakama nyingine kusikiliza mashauri kwa teknolojia hiyo,
Awali
teknolijia hiyo ilikuwa inatumika katika vituo sita, ambavyo ni mfumo
huo, umefungwa ambavyo ni Mahakama Kuu ya Tanzania katika Kanda za Dar
es salaam, Mbeya, na Bukoba pamoja na Kituo cha Mafunzo cha Kisutu,
Gereza la Keko na Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA), Lushoto.
Shauri likiendeshwa
kwa Mahakama Mtandao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...