Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MAWAZIRI wa Sekta wa Kilimo,Mifugo,Uvuvi pamoja wa nchi zilizo Kusini Mwa Jangwa la Sahara (SADC) zimekubaliana kufanya tathimini ya miezi mitatu madhara yaliyotokana na majanga mbalimbali ikiwemo na ugonjwa wa Virusi vya Corona ili kuweza kusaidia Sekta hiyo kuimarika.

Akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Sekta ya Kilimo, Mifugo,Uvuvi na Usalama wa Chakula ambaye ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema kuwa Mkutano huo wameazimia kufanya tathimini ya Sekta ya Kilimo,Mifugo,Uvuvi na Usalama wa Chakula kutokana na majanga mbalimbali  ikiwemo na Ugonjwa wa Virusi vya Corona ili kufanya Sekta hiyo kuimarika kuchangia Maendeleo kwa nchi wanachama.

Waziri Mpina ameongoza Mkutano huo kwa Njia ya Video Call kwa 11 za SADC zilizoweza kuingia katika mtandao.

Waziri huyo amesema kuwa baada ya kufanya tathimini hiyo wataangalia nchi ambazo zimepata  changamoto  kuweza kusaidiwa na nchi ambazo zimekuwa na ziada ikiwemo chakuala.

Mpina amesema kuwa kwa nchi ambazo hazina bahari na maziwa wameadhimia kuazisha ufugaji wa viumbe maji ili kwenda na Kasi ya upatikanaji vitoweo na hatimaye kuimarisha Afya wananchi kwa nchi wanachama wa SADC.

Waziri Mpina amesema kuwa Mwenyekiti wa SADC Rais John Pombe Magufuli yuko bega kwa bega kuhakikisha vikao vyote vinafanyika licha ya kuwepo kwa ugonjwa wa Virusi vya Corona kwa kutumia ushauri wa mawaziri wa Afya kufanya kwa kutumia Mawasiliano ya video call.

"Tumeadhimia kila kitu kilichojadiliwa kinapatiwa ufumbuzi ili kuleta Maendeleo ya wananchi wetu katika kufikia malengo kwa nchi wanachama wa SADC"amesema Mpina.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza na waandishi wa Habari mara baada kufunga Mkutano wa  Mawaziri wa SADC katika Sekta ya Kilimo,Mifugo,Uvuvi na Usalama wa Chakula iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimi Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa ,Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Kilimo mara baada ya kuhitimisha Mkutano wa SADC wa Mawaziri wa Sekta ya Kilimo Mifugo, Uvuvi na Usalama uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel akiongoza mada katika Mkutano wa SADC kwa Sekta ya Kilimo,Mifugo,Uvuvi na Usalama wa Chakula uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kwa Njia ya video call
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akifungua Mkutano wa Mawaziri wa SADC katika Sekta ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Usalama wa Chakula iliyofanyika jijini Dar  es Salaam kwa Njia ya video Call.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...