MFANYABIASHARA, Edgael Lema (43) mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka nane likiwemo la kukutwa na magogo yenye thamani ya  zaidi ya Sh. Milioni 383.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Vicky Mwaikambo na Wakili wa serikali mwamdamizi, Maternus Marandu imedai mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu, kusafirisha magogo,  kugushi,  kutoa nyaraka za uongo, kukwepa kodi na utakatishaji wa fedha

Akisoma hati ya mashtaka wakili Marandu amedai kati ya Novemba 2015 na Januari 2016 maeneo yasiyojulikana nchini Tanzania mshtakiwa huyo akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani walijipanga kuongoza genge la uhalifu huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Pia imedaiwa siku hiyo katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam mshtakiwa na wenzake hao ambao bado hawajakamatwa,  walisafirisha kontena 18 zenye vipande vya magogo 5296 aina ya mkurungu yenye thamani ya Sh 383,140, 840 ambazo ni mali ya serikali ya Tanzania bila ya kupewa kibali kutoka kwa mkurugenzi wa maliasili.

Aidha mshtakiwa huyo alitengeneza nyaraka za uongo wakijaribu kuonyesha kuwa imetolewa na ofisi ya Serikali ya Zambia huku wakijua siyo kweli.

Katika shtaka la tano na sita tarehe iimedaiwa, Siku isiyojulikana maeneo ya makao makuu ya Bandari ya Dar es Salaam iliyopo wilaya ya Ilala mshtakiwa huyo akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani hapo wakijua ni udanganyifu walitoa nyaraka za uongo kwenye ofisi hiyo wakionyesha nyaraka hizo zimetolewa na ofisi ya Serikali ya Zambia huku wakijua siyo kweli..

Imedaiwa kuwa, kati ya Novemba 2015 na Januari 2016 maeneo ya jiji la Dar es Salaam mshitakiwa huyo akiwa na nia ya kukwepa kodi alitoa nyaraka za uongo ili kukwepa kulipa kodi ya Sh 383, 140, 840 huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Katika shtaka la mwisho kati ya Novemba 2015 na Januari 2016 jijini Dar es Salaam mshtakiwa huyo alijipatia Sh 383, 140, 840 huku akijua kwamba fedha hizo zilikuwa zimetokana na zao la kosa la uhalifu wa kukwepa kulipa kodi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 21 mwaka huu mshtakiwa amerudishaa rumande kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...