Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Klabu ya Simba kwa kushirikiana na Taasisi ya Mo Dewji  imehitimisha zoezi la ugawaji wa Barakoa kwa wakazi wa maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam.

Zoezi hilo limehitimishwa kwa watendaji wa taasisi hiyo kukabidhi barakoa kwa ajili ya kujilinda na homa kali ya Mapafu (COVID-19) inayosababishwa na virusi vya corona.

Ikiwa ni siku ya tatu toka kuanza kwa ugawaji wa barakoa hizo, wananchi wamefurahia zoezi hilo la kuwakumbuka wananchi hususani wale ambao hawana uwezo wa kununua wenye kipato cha chini.

Barakoa zimekuwa zikishauriwa kutumiwa kama njia ya kupunguza uwezekano wa kusambaza virusi hivo pale ambapo mtu atakua ana kohoa ama kupiga chafya pamoja na kupunguza umbali ambao maji maji hayo yanaweza kuruka.

Barakoa hizo zimetengenezwa hapa nchini na kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited kwa kutumia pamba inayolimwa hapa nchini. Barakoa hizi ni imara na hivo kuruhusu uwezekano wa kutumika zaidi ya mara moja baada ya kufuliwa na kupigwa pasi.

Klabu ya Simba imeendelea kuchukua tahadhari kwa kuwalinda wachezaji wake na zoezi hili limekua na lengo la kuwakumbuka wananchi na mashabiki wake pamoja na kuwasihi waendelee kufuata hatua zinazoelekezwa.

Taasisi ya Mo Dewji  imejitolea barakoa 25,000 kwa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa kurudisha kwa jamii kwa kuangalia namna bora ambazo inaweza kusaidia katika mapambano dhidi virusi vya corona. Hususani kwa wananchi wa kawaida kuweza kujilinda na kupambana na virusi hivo.

Ugawaji wa barakoa hizo umefanyika katika masoko na vituo vya boda boda mbali mbali jijini Dar es Salaam ikiwemo maeneo ya Kivukoni, Kariakooo, Tandale, Manzese, Buguruni, Makumbusho, Mabibo, Temeke, Mbagala, Msasani, Kimara, Mbezi na Tegeta. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...