MWANAMKE Angellah Kiwia na Mohamed Rushaka wakazi wa jijini Dar es salaam wamfikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka manne yakiwemo kutoka nyara na kutakatisha fedha

Washtakiwa hao ambao wamesomewa mashtaka yao leo Mei 11, 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rashid Chaungu wanadaiwa kuwa, kati ya Machi 1 na 31, 2020 katika maeneo tofauti Jiji la Dar es Salaam, kwa makusudi waliongoza genge la uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo 

washtakiwa hao walimteka Seleman Mohamed huku wakiwa na nia ya kumpeleka katika hatari ya kumuumiza wakimtishia kumuua  huku wakimshinikiza awalipe kiasi cha milioni 30 wanazomdai. 

Aidha katika shtaka la nne la kutakatisha fedha imedaiwa katika tarehe zilizotajwa awali jijini Dar es Salaam, washtakiwa walijipatia  Sh milioni 30 kutoka kwa Mohamed, huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la makosa tangulizi ya uhalifu wa kuteka nyara

Awali kabla ya kusomewa mashtaka hakimu Chaungu aliwaeleza washtakiwa kuwa hawataruhisiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Chaungu ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 25, mwaka huu, washtakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu mashtaka yanayowakabili hayana dhamana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...