Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Mwanza wakiandaa mizigo ambayo ni minofu ya samaki ya kilogram 17,262 iliyosafirishwa na Ndege ya Ethiopia  Airlines iliyoanza safari zake 21 mei 2020 kuja Tanzania katika mkoa wa Mwanza  kuchukua minofu ya samaki. Tarehe 21 mei 2020.

 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya{kulia} akikagua uandaaji wa mizigo ya minofu ya samaki  ya kilogram 17,262 zenye thamani ya Tsh. 191,874,837.78 iliyopelekwa ndege ya Ethiopia  Airlines iliyoanza safari zake 21 mei 2020 kuja Tanzania katika mkoa wa Mwanza  kuchukua minofu ya samaki. Tarehe 21 mei 2020.
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya{kulia} akiwa na Naibu wa Ujenzi, Uchukuzi na Masiliano Mhandisi, Atashasta J Nditiye {aliyeva koti jeusi} pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella{kushoto} wakiwa katika katika shughuli ya mapokezi ya ndege ya Ethiopia  Airlines iliyoanza safari zake kuja Tanzania katika mkoa wa Mwanza  kuchukua minofu ya samaki za kilogram 17,262. Tarehe 21 mei 2020 . Picha na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara
 Ndege ya Ethiopia  Airlines iliyoanza safari zake 21 mei 2020 kuja Tanzania katika mkoa wa Mwanza  kuchukua minofu ya samaki na imepakia kilogram 17,262 zenye thamani ya Tsh. 191,874,837.78 na mrabaha uliolipwa ni Tsh. 9,541,301.21. Tarehe 21 mei 2020.
  
Na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya ametangaza fursa za soko la samaki kanda ya ziwa.

Mhe. Manyanya ameyasema hayo 21 mei 2020 katika shughuli ya mapokezi ya ndege ya Ethiopia Airlines iliyoanza safari zake kuja Tanzania katika mkoa wa Mwanza kuchukua minofu ya samaki ambao inauzwa katika nchi mbalimbali.

Mhe. Manyanya amesema kuwa "Mpaka kufikia mwezi machi 2020 samaki Tani 392,933 wamevunwa nchini na mauzo yameongezeka kulingana na miaka miwili iliyopita ambapo mauzo yalikuwa Bilioni 379 na kufikia bilioni 691.88 kwa mwaka 2018/2019. Tani 32,388.88 zenye thamani ya Bilioni 436.97 ziliuzwa nje ya nchi na mapato kwa Serikali yalikuwa bilioni 19.1"

Mhe. Manyanya baada ya kujionea ndege ya Ethiopia Airline ikipakia samaki ametumia fursa hiyo kuwatangazia na kuwadhihirishia wawekezaji wote nchini kuwa kuna soko la samaki la uhakika kwasababu kwa sasa samaki zinafatwa moja kwa moja mkoa wa mwanza na kupelekwa katika maeneo mbalimbali duniani kote.

“Tanzania tumejariwa, tunao samaki wazuri na wakutosha na sio ziwa victoria tu tuna majiziwa mengine makubwa na bahari ya hindi, kwa hiyo naomba niwadhihirishie wawekezaji wote kuwa sasa tuna soko la uhakika la samaki kwahiyo jitokezeni kuwekeza kwasababu minofu yetu ya samaki inafatwa moja kwa moja na ndege hadi mkoa wa Mwanza”

Aidha amesisitiza kuwa "Ndege ya Ethiopia iliyoanza kuja leo 21 mei 2020 imepakia kilogram 17,262 zenye thamani ya Tsh. 191,874,837.78 na mrabaha uliolipwa ni Tsh. 9,541,301.21 na samaki hizo zitauzwa katika nchi za Belgum, Holand, Germany, France, Portugal na Australia na kwa upande wa mabondo (fish maws) soko kubwa ni china"

Nae Naibu wa Ujenzi, Uchukuzi na Masiliano Mhandisi, Atashasta J Nditiye amesema kuwa safari za ndege ya Ethiopia kuja kuchukua samaki hapa mwanza ni fursa kubwa kwa wana Mwanza na Kanda ya ziwa kwa ujumla maana kabla ya hapo ilikuwa inakuja ndege ya Rwanda Air ambayo ilikuwa inakuja mara moja kwa wiki kila jumanne Lakini Ethiopia Airlines imeanza safari leo na bado ratiba yake haijajulikana.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amesema kuwa ni viwanda vitatu vilinavyosafirisha samaki leo ambavyo ni (i) Kiwanda cha Victoria Perch limited ambao wanasafirisha Tani 5.4 (5,400kg) zenye thamani ya USD 21,600 (ii) Kiwanda cha Nile Perch Limited amabo wanasafirisha Tani 8.9 (8990kg) zenye thamani ya USD 35,900 (iii) Kiwanda cha Omega Fish limited kinachosafirisha Tani 5 (5,000kg) zenye thamani ya USD 22,320.

Aidha, Mongella amesisitiza kuwa Uzakishaji wa kanda ya ziwa kwa wastani kila wiki katika kipindi cha mavuno ni wastani wa Tani 1100 na kipindi mavuno haba ni tani 220.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...