Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Shirika la ndege la Precision Air wamezindua safari  za ndege ya mizigo kutokea Tanzania na kuelekea Hahaya katika Visiwa vya Comoros wakipeleka bidhaa mbalimbali.

Safari hizo zimeanza rasmi siku ya Jumamosi kutokana na mabadiliko katika soko na nchi nyingi kufunga mipaka yao.

Akitoa taarifa hiyo,  Meneja Masoko na Mawasiliano amesema wamebadilisha moja ya ndege zao aina ya ATR72-500 kuwa ndege ya mizigo, na safari ya kwanza ilikuwa ni siku ya Jumamosi.
Amesema, kutokana na mabadiliko katika soko safari yao ya kwanza ya mizigo kuelekea Hahaya waliweza kusafirisha madawa pamoja na mbogamboga. 

Mremi ameeleza kuwa Kupitia safari hiyo ya kwanza pia wamezindua rasmi safari za mizigo ambapo zitakuwa zikifanyika kila Jumatano kuelekea Hahaya.

Mremi amesema, ndege hyo ya ATR72-500 ina uwezo wa kubeba tani 5.5 kwa wakati mmoja na itapeleka mahitaji muhimu kila wiki.

Aidha,  safari za ndani na kikanda zitaendelea kulingana na mahitaji.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...