Na Sultani Kipingo wa Michuzi TV
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa gumzo kubwa sana duniani kwa siku kadhaa sasa toka aongee mjini Chato wakati wa hafla fupi ya kumwapisha Mhe. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Augustine Mahiga aliyefariki Ijumaa iliyopita.
Vyombo vya habari vyote vikubwa duniani, kama vile televisheni  za CNN, Al Jazeera, Sky News, BBC, CBS, DW, VOA pamoja na magazeti ya New York Times, Financial Times, Daily Mail, The Guardian, Times of India na wakala wa habari Reuters, vimeandika habari zake hasa juu ya wasiwasi wake dhidi ya ufanisi katika maabara ya vipimo vya ugonjwa wa Corona.
Vyombo hivyo vya kimataifa, ambavyo daima vinashutumiwa kuandika mabaya tu kutoka barani Afrika, vimejikuta vikimuongelea Rais Magufuli ambaye amegusa hisia za kila mtu duniani wakati huu wa janga la Corona, akifanya viongozi na wanasayansi kuzikodolea macho upya mashine za kupimia ugonjwa huo.
Rais Magufuli amesisimua dunia zaidi pale aliposema sampuli kadhaa  zilipelekwa kwenye maabara kuu ya Taifa  bila ya wataalamu wa maabara hiyo kujua kuwa si za binadamu, ambapo sampuli ya papai iliyoitwa Elizabeth ilikutwa na corona, sambamba na sampuli za ndege kwale pamoja na mbuzi kukutwa na corona pia. 
“…Papai lile lipo halijafa linaiva tu. Mbuzi yule yupo tu hajafa, fenesi lile lipo tu labda lije kuoza…kwa hiyo natoa wito kwa Watanzania msiwe na hofu…mbona mafua yamekuwepo lakini haya ni makali, nayo yatapita..." amenukuliwa Rais Magufuli na vyombo hivyo vya kimataifa.
Vyombo hivyo vimeendelea kumnukuu Rais Magufuli akisema "…Lazima ugundue kuna mambo ya ajabu yanafanyika nchi hii. Ama wahusika wa maabara wamenunuliwa na mabeberu, ama hawana utaalamu jambo ambalo si kweli kwa kuwa maabara hii imetumika sana katika magonjwa mengine. Ama zile sampuli zinazoletwa maana vifaa vyote vinatoka nje, hivyo lazima kuna kitu fulani kinafanywa," 
Rais Magufuli, ambaye hadi sasa anatajwa kuwa Rais wa Afrika anayeheshimika sana duniani kwa misimamo wa kutoyumbishwa na mtu ama Taifa lolote na kuona mbali, alisema kutokana na taarifa hizo anaamini kuna watu ambao walipewa majibu yasiyo sahihi, na kwamba lazima kuna watu wameambiwa kuwa wao ni “positive lakini si wagonjwa wa corona, na kwamba inawezekana wengine wakafa kwa hofu.
Rais Magufuli pia alivishutumu vyombo vya habari vya kimataifa kwa namna vinavyoripoti kuhusu janga hilo nchini Tanzania licha ya kuwa vyombo hivyo vipo katika maeneo ambayo yameathirika zaidi ya Tanzania na zinaongoza duniani kwa kuwa na waathirika wengi.

Monicah Wakio, mtafiti na mwanasayansi wa Kenya anayefanya kazi katika Wuhan Viral Research Centre nchini China, amemsifia Rais Magufuli kuwa ni mtu smart na asiyeyumbishwa na mtu lakini anayechukiwa kwa msimamo wake wa kustukia dili la Magharibi la kusambaza hofu juu ya Corona ili wafanikishe agenda zao.
"Ugonjwa wa corona hauwezi kuwa mbaya zaidi ya HIV, Kansa, Ebola au Sars. Naongea kama mwanasayansi wa mambo ya virusi hapa Wuhan Institute of Virology. Corona ni kweli haina tiba kama ilivyo kwa mafua ya kawaida ambayo pia hjayana tiba. Hivyo corona isifanywe kuwa ni dili. Na hilo Magufuli analijua" amesema Monica Wakio.
Akizungumzia Rais wa Madagascar Andry Rajoelina kutangaza kwamba taifa lake limezindua dawa ya mitishamba ya kutibu Covid-19, Rais Magufuli amesisimua watu zaidi pale aliposema atatuma ndege nchini humo kuchukua hizo dawa ili zije kutumika na Watanzania. 
 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...