Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametangaza Punguzo kubwa la Bei ya Nguo la hadi 80% kwenye Maduka Makubwa ya Nguo yaliyopo Jijini humo ili kuhakikisha Wananchi wanapendeza na kuwa nadhifu Jumapili ya May 24 kwenye Kilele cha Siku Tatu za Shukrani Kwa Mungu zilizotangazwa na Rais Dkt. John Magufuli.

RC Makonda amesema Miongoni mwa Maduka Makubwa yaliyoamua kutoa punguzo la bei ni pamoja na Mr. Price na Red Tag ya Mlimani city, Vunja Bei, Maduka yaliyopo City Mall pamoja na Maduka Mengine yaliyopo Posta, Kariakoo, Kinondoni na Sinza.

Aidha RC Makonda amesema atafurahi kuona kila mwananchi wa mkoa huo anasheherekea kwa nderemo na vifijo siku ya jumapili kama sehemu ya shukrani kwa Mungu kwa kutukinga na Corona na baada ya hapo kila mmoja achape kazi ili kwa pamoja tuinue Uchumi wa Taifa.

Pamoja na hayo RC Makonda ametangaza Shindano la DJ bora ambapo kila DJ atatakiwa kumtumia Video Clip huku akiwaelekeza wenye Bar, Hotel, Lodge, Band na Biashara kuzifungua.

Kwa Upande wao wamiliki wa Maduka ya Mr. Price, Red Tag na Maduka Mengine wamewakaribisha Wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya manunuzi huku wakimpongeza RC Makonda kwa kuwapigania Wananchi wa mkoa huo ili kuhakikisha wanapata mavazi mazuri kwa bei nafuu.

RUDINI DAR KUMENOGA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...