Na Amiri kilagalila,Njombe
CHAMA cha Msalaba Mwekundu (RED CROSS TANZANIA) wamezindua mpango wa utoaji elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona mkoa wa Njombe,ili kukata mnyororo wa maambukizi ya virusi hivyo nchini Tanzania.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa zoezi hilo,Rais wa Tanzania red cross Society David Kihenzile,amesema kwa kuwa serikali ilishaanza kufanya kazi ya uelimishaji lakini wao kama Chama wameona haja ya kuongeza nguvu kama wasaidizi wa serikali katika utoaji wa huduma za kibinadamu.

Kihenzile amesema wanaendelea na zoezi hilo la utoaji wa elimu karibu mikoa yote nchini huku mpaka sasa mikoa isiyozidi mitatu ikiwa bado haijafikiwa na lengo likiwa ni kufikia mikoa yote nchini.

Amesema kwa mkoa wa Njombe wanakwenda kuvifikia vijiji vyote 381 na mitaa yake 82 ili kuiongezea nguvu seriklai kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii

“Tutakwenda kufikia katika mkoa wote wa Njombe kwa maana wilaya zote na halmashauri zake sita,kata 107,tarafa 18,tutafikia vijiji 381 na mitaa yake 82,tutafikia maeneo ya umma na ya mikusanyiko ili kuiongezea nguvu serikali kwenye kutoa elimu kwa jamii,na hatuendi kuongeza neon kwa kuwa jumbe imeshapangwa na wizara ya afya kwa hiyo sisi tunaenda kupaza sauti”alisema David Kihenzile

Simon M Kadogosa ni meneja Tathmini Magonjwa ya Mlipuko kwa niaba ya Katibu wa Red Cross Tanzania,ameendelea kuwasihi watanzania kupokea maelekezo ya wataalamu wa afya dhidhi ya kujikinga na virusi vya Corona huku akibainisha kuwa miongoni mwa nyenzo watakazozitumia katika kutoa elimu ni pamoja na mabango yenye jumbe za maandishi,vipeperushi pamoja na vipaza sauti.

“Tutaunga mkono jitihada za serikali za utoaji elimu kwa jamii kwa kuleta mabango 4000 yatakayobandikwa maeneo tofauti ndani ya halmashauri zote kwa mpango jumuishi,tuna vipeperushi elfu kumi na nne pia vitakavyogawiwa mkoa mzima,lakini pia watumishi wa kujitolea wa Red Cross watatumia vipaza sauti kwenye maeneo ya kimkakati kuhakikisha zile jumbe za sauti za watu wasio jua kusoma wanaziskia na kuzifanyia kazi”alisema Kadogosa

Naye Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa mpango huo katika ukumbi wa chuo kikuu huria uliopo kwenye maeneo ya ofisi za mkoa wa Njombe,amesema mapambano ya Corona sio viongozi bali ni kila mwananchi hivyo ni lazima kila mwananchi apambane huku akifanya kazi.

“Elimu kwetu inaendelea lakini lazima tuamini Mungu,na sisi huku tumeongeza nguvu kwa maneno matatu ya Sala,tahadhari na kazi,na lazima tuchape kazi ili ugonjwa ukiondoka au ukiendelee tusije kujikuta tupo kwenye anguko la kiuchumi”

Vile vile Ruth Msafiri ameendelea kuhamasisha watoa huduma katika kusanyiko kuvaa barako huku akipiga marufuku kwa taasisi na watoa huduma kuto kutoa huduma kwa mtu asiyevaa barakoa wakati alipofuata huduma.
Rais wa Tanzania red cross Society David Kihenzile akizungumza na wanachama wa Red Cross mkoa wa Njombe kabla ya uzinduzi wa zoezi la utoaji wa elimu ya kujikinga na Corona.
Wanachama wa Red Cross wakifanya mazoezi katika maeneo ya ofisi za mkoa wa Njombe mara baada ya zoezi la uzinduzi wa mpango wa utoaji elimu.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akishika mabango yatakayotumika wakati wa uelimishaji wa jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...