MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto akiwakabidhi baadhi ya wawakilishi wa Taasisi kubwa za Dini Jijini Tanga msaada wa vifaa vya usafi ambayo vimetolewa na taasisi ya odo Ummy Foundation inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia mwenye kanzu ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Waalimu wa Kiislamu Tanzania ya Tamta Mohamed Mohamed Zikri akifuatiwa na Mwakilishi kutoka Katoliki Chumbageni John Maembe kushoto anayeshuhudia ni Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Khatibu Kilenga 

  MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto akiwakabidhi baadhi ya wawakilishi wa Taasisi kubwa za Dini Jijini Tanga msaada wa vifaa vya usafi ambayo vimetolewa na taasisi ya odo Ummy Foundation inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia mwenye kanzu ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Waalimu wa Kiislamu Tanzania ya Tamta Mohamed Mohamed Zikri akifuatiwa na Mwakilishi kutoka Katoliki Chumbageni John Maembe kushoto anayeshuhudia ni Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Khatibu Kilenga

 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo ambao umetolewa na Taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa Taasisi Kubwa za Dini Jijini Tanga 

 Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Khatibu Kilenga kulia akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa mara baada ya makabidhiano ya vifaa hivyo



 Sehemu ya vifaa ambavyo vimetolewa na Taasisi ya Odo Ummy Foundation



TAASISI YA Odo Ummy Foundation leo wamekabidhi msaada wa vifaa vya usafi kwa Taasisi kubwa za Dini ya Kiislamu na Kikristo Jijini Tanga ikiwa ni kuhimiza usafi katika jamii kwa kupitia taasisi hizo kutokana na maeneo yao yanakuwa na mikusanyiko mikubwa ya waumini.

Msaada huo umekabidhiwa leo kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Khatibu Kilenga alisema kwamba wameona watoe msaada huo kupitia Taasisi hiyo ambayo ipo chini ya Mwenyekiti wao na Mwasisi Ummy Mwalimu ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto.

Alisema kwamba taasisi hiyo imeamua kutoa msaada huo kwenye taasisi hizo za dini kutokana na kwamba kunakuwa na mikusanyiko mikubwa ya waumini ambao wanakwenda kufanya ibada hivyo wanahitaji nao kuweza kuhakikisha wanazingatia suala la usafi ambalo ni muhimu.

“Taasisi yetu imekuwa ikisaidia jamii kwenye masuala mbalimbali ikiwemo kujenga afya ya jamii na kama tunavyojua afya ni pamoja na usafi na kwa sababu kuna magonjwa na mambo mbalimbali yanaendelea kwenye jamii hivyo taasisi yao kama walivyokuwa wakitoa sapoti kwenye jamii na ndio maana tumeona tutoe vifaa vya kusaidia kulinda usafi kwa Taasisi hizo “Alisema

“Hivyo leo tumetoa matenki kwa taasisi kubwa za dini ya kiislamu na dini ya kikristo tumegawa kwenye taasisi hizo kwa sababu zina mkusuanyiko mikubwa wa waumini …vifaa hivi vitakwenda kuwa chachu ya kuimarisha usafi kwenye maeneo yenu tunajua vipi lakini tunajua havitoshi ndio maana tumeona tusaidie kwenye maeneo ya dini ingawa tunasapoti pia kwenye maeneo mengine”Alisema Katibu huyo.

Hata hivyo alisema baada ya vifaa hivyo kukabidhiwa baadae watavisambaza kwenye taasisi mbalimbali ili kuwawezesha kuvitumia kwa ajili ya kuhakikisha wanakuwa kwenye hali ya usafi wao na waumini wao wanaokwenda kufuata ibada kwenye maeneo hayo.

Awali akizungumza wakati akipokea msaada huo kwa niaba ya taasisi hizo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliishukuru taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa kusaidia jamii kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwenye jamii ambavyo vimekuwa ni chachu ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza kwenye maeneo mbalimbali.

Alisema msaada huo umekuwa wakati muafaka ambapo jamii inapaswa kuhakikisha wanakuwa safi wakati wote kwa kunawa mikono wanapokuwa wakiingia maeneo mbalimbali hivyo Odo Ummy ameweza kusaidia harakati hizo za kukabiliana nalo.

“Leo natoa shukrani mara ya pili kwa Taasisi hii kwani imekuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Jiji la Tanga kwa kutoa misaada mbalimbali awali walikwisha kutoa lakini kwa sasa wameona watoe tena kusaidia jitihada za serikali kuhakikisha wananchi wanazingatia usafi kwenye maeneo mbalimbali”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba Corona sio ugonjwa pekee ambao mapambano yake tutayashinda kwa usafi hivyo mapambano yaendelea kwa sababu hata ikiondoka yapo magonjwa yanayofanana nayo hata ikiondoka lakini bado wananchi wanahitajika kuzingatia usafi kwa ajili ya magonjwa mengine ambayo kuenea kwao yanatokana na uchafu.

Naye kwa upande wake Katibu Mkuu wa Taasisi ya Waalimu wa Kiislamu Tanzania ya Tamta Mohamed Mohamed Zikri aliishukuru Taasisi ya Odo Ummy Foundation huku wakimuomba mwenyezi Mungu kuendelea kuwapa mafanikio ili waendelee kuwajali.

Alisema kwamba imani yao Mwenyezi Mungu hawezi kuacha ugonjwa huo kuendelea milele yatakuwa kama yalivyokuwa mengine ya mlipoko na wenyewe utafikia mwisho huku akiwataka viongozi wa dini kuchukua tahadhari kubwa kwa kuwaeleza wenzao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...