JUMUIYA
ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilayani Hanang'
Mkoani Manyara, kupitia kampeni yao ya mikono safi Hanang' salama
wameikabidhi Serikali vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya
corona vya thamani ya sh. 531,000.
Makamu
Mwenyekiti wa kampeni ya mikono safi Hanang' Emmanuel Gamasa
akizungumza jana alisema lengo la UVCCM wilayani humo kukabidhi msaada
huo wa vifaaa hivyo ni kuiunga mkono serikali katika mapambano ya
kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.
Gamasa
alisema wao kama UVCCM wilayani humo kupitia kampeni ya mikono safi
Hanang' salama wametoa vifaa hivyo vya kujikinga na corona kwa thamani
ya sh. 531,000 kwa ajili ya wananchi wa eneo hilo kutumia.
Alisema
wametoa ndoo 30 za kunawa mikono na vitakasa mikono lita tano ili
kuiunga mkono serikali katika mapambano hayo dhidi ya corona.
Mganga
mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Hanang' Dk Boniface Manditi
aliwashukuru UVCCM wilaya ya Hanang' kwa kuona uhitaji wa kujikinga na
kuweza kuwajali wahitaji.
Dk
Manditi alisema tahadhari zinazochukuliwa ni za muhimu kuliko hatua za
kufunga mipaka, hivyo watu waendelee kunawa mikono kwa maji tiririka kwa
sabuni, kuvaa barakoa na kufanya kazi.
''Hivi
mlivyotusaidia leo tunashukuru sana na itaendelea kutuweka katika
sehemu nzuri ya mapambano dhidi ya janga hili corona,'' alisema Dk
Manditi.
Katibu Tawala wa
wilaya ya Hanang' Paulo Bura baada ya kupokea msaada huo aliwashukuru
UVCCM na kusema ni mfano wa kuigwa kwani bado kuna uhitaji wa vifaa
hivyo.
''Siyo kuwa vijana
wana fedha ila wakaona waguse kile kidogo walichonacho ili kufanikisha
jukumu hili muhimu la kuunga mkono serikali yao katika mapambano ya
janga hili la corona,'' alisema Bura.
Aliwahakikishia
vijana hao kuwa serikali ipo pamoja nao bega kwa bega na juhudi
wanazozifanya kama UVCCM wanazitambua na vifaa walivyotoa vitatumika kwa
makusudi yaliyokusudiwa.
''Vifaa
hivi tunavikabidhi kituo cha afya cha Katesh ni imani yangu wataalamu
wataangalia maeneo yote muhimu na kuweka ili ziweze kuwasaidia wananchi
walio wengi, matarajio ya matunda na matokeo ya vifaa hivi yaweze
kuonekana,'' alisema Bura.
Mwenyekiti
wa kamati ya uhamasishaji na maafa wa UVCCM mkoani Manyara, mwalimu
Carol Gisimoy alisema hiyo ni awamu ya kwanza ya kumuunga mkono Rais
John Magufuli katika mapambano dhidi ya janga la corona.
Mwalimu
Gisimoy alisema UVCCM Hanang' wametekeleza maelezo yaliyotolewa na
Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally ya kuitaka jumuiya hiyo kusimama
mstari wa mbele kutoa elimu na tahadhari zinazoelezwa na Serikali
kupitia Wizara ya Afya.
Hata
hivyo, aliwapongeza vijana wote walioshiriki shughuli hiyo na wadau
wengine bila kuwasahau madaktari na wauguzi wanaokesha kuhakikisha jamii
inaendelea kuwa salama.
Wadau na wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM
(UVCCM) Wilayani Hanang' Mkoani Manyara, baada ya kumkabidhi ndoo 30 za
kunawa mikono na vitakasa mikono lita tano za thamani ya shilingi
531,000 kwa Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Paulo Bura kwenye kituo cha
afya Katesh jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...