Shindano
la Tusua mapene na Vodacom linaloendelea kote nchini, linawawezesha
watumiaji wa mtandao wa Vodacom kuweza kujishindia kitita cha milioni 10
kila wiki na wengine waliobaki watajishindia zawadi ndogo ndogo. Hili
ni shindano lilioanza mwaka 2017, na kuendelea kuwanufaisha wateja wa
Vodacom nchini.
Ili
kushiriki kwenye promosheni hii, mteja anatakiwa kutuma neno “CHECK” au
“VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.
Unaponunua
tiketi, moja kwa moja unaingia kwenye droo, washindi wa droo wanaingia
kwenye Mpambano ambapo wanatumiwa neno maalum " keyword " watakayoituma
kwenda 15544 ili kuweza kukomboa zawadi. Wa kwanza kutuma neno hilo
ataibuka na kitita cha shilingi milioni 10, na wengine wanajipatia
zawadi ndogo ndogo.
Akikabidhi
mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 za kitanzania,
Meneja Mauzo mwandamizi wa Vodacom kanda ya Kaskazini, Abednego Mhagama
alimpongeza mshindi na kuhamasisha wateja kushiriki Zaidi ili kuweza
kujishindia zawadi kemkem.
Nae
mshindi wa zawadi ya Tusua mapene kutoka Arusha mjini, Mfanyabiashara
Neema Laiser aliwashukuru Vodacom kwa kuanzisha shindano hili ambalo
limemuwezesha kujishindia pesa itakayomuwezesha kuongeza mtaji na hivyo
kuimarisha biashara yake.
"Kwa
kweli sikuamini nilipopigiwa simu nikajua mambo ya uwongo, lakini kumbe
ni kweli na nawashauri watu wasiache kutumia mtandao wa Vodacom maana
ushindi kama huu unaweza kukukwamua kiuchumi" alisema Laiser.
Mshindi
wa wiki wa shindano la TUSUA MAPENE NA VODACOM, Neema Laiser (
katikati) mfanyabiashara, mkazi wa mtaa wa Uswahilini Jijini Arusha,
akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 toka
kwa Meneja mkakati wa Masoko Vodacom kanda ya Kaskazini, Abednego
Mhagama (kulia) na Meneja Mauzo mwandamizi wa Vodacom kanda hiyo,
Nathanael Pedigando
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...