NA TIGANYA VINCENT

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watumishi wote waliopewa mashine za kukusanyia mapao (POS) ambao hadi hivi wadaiwa mapato waliyokusanya kwa kutoyawasilisha Benki.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa kikao cha robo ya tatu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Urambo.

Alisema kitendo hicho ni kinyume cha kifungu cha 60 cha Sheria ya fedha za umma yam waka 2001.

Makungu alisema dosari za aina hiyo ndio zimekuwa zikisababisha upotevu wa fedha za umma na kuziagiza Halmashauri kuhakikisha zinasimamia kwa ajili ya kuziondoa.

Aidha Katibu Tawala huyo wa Mkoa amepiga marufuku kwa Wakurugenzi na Waweka Hazina kuruhusu utaratibu wa Wakusanyaji mapato kuchukua asilimia zao(commission) kutoka makusanyo ya fedha za mapato ya ndani kabla ya kupelekwa Benki.

Alisema vitendo hivyo vinasababisha matumizi ya pesa ‘mbichi’ na kupelekea Halmashauri kupoteza mapato yake na kusababisha uzalishaji wa hoja za kiukaguzi.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora ameziagiza Menejimenti za Halmashauri zote za Mkoa huo kuhakikisha hazizalishi madeni yanayotokana na stahili za watumishi wanahama na wale wanaopandishwa madaraja.

Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alishaagiza hakuna mtumishi atayehamishwa bila kulipwa stahili na kuongeza kuwa kwenda kinyume cha hapo ni kutenda kosa.

Makungu aliongeza kuwa kuchelewa kulipa stahiki za watumishi kunavunja morali ya kufanyakazi jambo ambalo linaweza kusababisha mgawanyiko miongoni mwa Watumishi.

Aidha Katibu Tawala huyo aliagiza Halmashauri zote kuanza kuandaa stahiki za posho za Madiwani ili Mabaraza yatakapovunja wasipate usumbufu wa kufuatilia. 
 Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakiwa jana katika kikao cha robo ya tatu huku wakiwa wamechukua tahadhari ya kujikinga na Virusi vya Corona.
 Katibu Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akihutubia jana  kikao cha robo ya tatu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Urambo.
 .Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa akichangia hoja wakati wa  kikao cha robo ya tatu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Urambo kilichofanyika jana.Picha na Tiganya Vincent
Ofisi ya RC Tabora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...