JESHI LA POLISI (M) MWANZA LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA 13 KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MAKOSA MBALIMBALI BAADA YA KUFANYA OPERASHENI KALI YA KUZUIA VITENDO VYA UHALIFU NA KUWAKAMATA BAADHI YA WATU WANAOJIHUSISHA NA VITENDO HIVYO.

TUKIO LA KWANZA-; KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA MAUAJI YALIYOHUSISHA RAMLI CHONGANISHI.

TAREHE 02.05.2020 MAJIRA YA 02:00HRS USIKU KATIKA KITONGOJI CHA IMALANGE, KIJIJI CHA MWANANGWA, WILAYA YA MISUNGWI, MKOA WA MWANZA, ALIKAMATWA MTUHUMIWA WA KOSA LA MAUAJI AITWAYE RODHA SHABANI, MIAKA 27, MSUKUMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA MWANKALI, AMBAYE BAADA YA KUHOJIWA KWA KINA ALIKIRI KUHUSIKA NA MAUAJI YA BIBI KIZEE NDEBETO TABITHA KAKULA, MIAKA 78, MSUKUMA, MKULIMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA MWANKALI, ALIYEUAWA TAREHE 29.04.2020 MAJIRA YA 08:20HRS, KWA KUKATWA NA KITU 

CHENYE NCHA KALI AMBACHO BAADAE ILIBAINIKA KUWA NI PANGA SEHEMU YA SHINGONI UPANDE WA KULIA WAKATI AKITOKA KISIMANI KUCHOTA MAJI. TUKIO HILO LILITOKEA BAADA YA MGANGA WA KIENYEJI AITWAYE MUHANGWA PAUL KUMPIGIA RAMLI CHONGANISHI MTUHUMIWA ALIYEMUUA BIBI KIZEE HUYO KWA MADAI ALIWAROGA WATOTO WAKE WAWILI NA KUSABABISHA VIFO VYAO. UPELEZI UMEWEZESHA KUKAMATWA KWA MGANGA HUYO WA KIENYEJI NA PANGA LILILOTU--MIKA KWENYE UHALIFU HUO LIMEPATIKANA. UPELELEZI WA SHAURI HILI UMEKAMILIKA KWA ASILIMIA 90 NA WATUHUMIWA WOTE WATAFIKISHWA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO.

TUKIO LA PILI; - KUKAMATWA KWA MAMA ALIYE TELEKEZA WATOTO KWENYE MAZINGIRA HATARISHI YA MAJALUBA YA MPUNGA.

TAREHE 29.4.2020 MAJIRA YA 06:00HRS ASUBUHI HUKO NYAKATO, WILAYA YA ILEMELA, MWANAMKE AITWAYE HAPPINES MAFURU, MIAKA 23, MJITA, MKULIMA NA MKAZI WA NYAMHONGOLO, ALIKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO LA KUTELEKEZA WATOTO WAWILI LILILOTOKEA TAREHE 27.04.2020 MAJIRA YA 05:00HRS KATIKA MASHAMBA YA MPUNGA (MAJARUBA), TUKIO HILO LILITOKEA MTAA WA MTAKUJA, NYAMHONGOLO, WILAYA YA ILEMELA, AMBAPO WATOTO HAO WALITELEKEZWA. MAJINA YA WATOTO NI 1. KELVIN MATHIAS, UMRI MWAKA MMOJA NA MIEZI 7 NA 2. ANASTAZIA MATHIA, UMRI MIEZI 4. WATOTO WANAENDELEA VIZURI, HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO.

JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UPELELEZI WA KINA ILI KUJUA MAZINGIRA YA TUKIO HUSIKA YAKOJE IKIWA NI PAMOJA NA KUENDELEA KUMSAKA MZAZI MWENZAKE ALIYETOROKA.BAADA YA TUKIO HILI.

TUKIO LA TATU:-
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KATIKA KIPINDI CHA KUANZIA MWEZI MARCH, 2020 HADI MWEZI APRIL 2020, KATIKA MAENEO YA JIJI LA MWANZA, LILIENDESHA OPERESHENI KALI DHIDI YA WAHALIFU WA MATUKIO YA UVUNJAJI WA NYUMBA USIKU NA WIZI WA VIFAA VYA NYUMBANI VYA KI ELEKTRONIK, AMBAPO KATIKA OPERESHENI HIYO WATUHUMIWA 7, PAMOJA NA FLAT TV 30, MOTA ZA MACHINE 2, DEKI 2, SUBWOOFER 2 NA VIFAA VYA KUVUNJIA KAMA VILE NYUNDO, SHOKA, NONDO, SIMU 30,TINDO, SPANA, PLAIZI, BARUTI NA VIFAA VYA KULIPULIA VIMEKAMATWA.

WATUHUMIWA WANAOSHIKILIWA NI;-
JUMA SAID MIAKA 35, MUHA, MKAZI WA KIRUMBA.
SAITOTI MAKOKOYO, MIAKA 28, MASAI, MKAZI WA BWIRU.
KELVIN IRIZIKIWA, MIAKA 32, MUHA, MKAZI WA BWIRU.
HUSSEIN MASOUD, MIAKA 42, MNYAMWEZI, MKAZI WA ISEVYA –TABORA.
KIROBA HEKA, MIAKA 38, MSUKUMA, MKAZI WA NAKATUNGURU.
KUDRA MELIKIADI, MIAKA 23, MJITA, MKAZI WA NAKATUNGURU.
BUSUMBILO CHARLES, MIAKA 25, MJITA, MKAZI WA KAMKOKO.

SIMON DEONATUS @ KILLER, NAMAGUBO.
ALLY BAKARI, MIAKA 24, MJITA, MKAZI WA MDOE.

JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UPELELEZI WA MASHAURI HAYO, MARA BAADA YA KUKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA LINAWATAKA WANANCHI WOTE WALIOWAHI KUIBIWA TV NA VIFAA VINGINE VILIVYOTAJWA WAFIKE KITUO CHA POLISI KATI ILEMELA NA NYAKATO KWA UTAMBUZI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA KUWASHUKURU WANANCHI WOTE WANAOENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAKAMATWE NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA. PIA LINAWATAKA WANACHI KUACHA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI HAZINA USTAWI KWA JAMII.

IMETOLEWA NA:
Muliro JUMANNE MULIRO -; ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
04 MAY, 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...