Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imemwita Dk. Imni
Patterson, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa lengo la
kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa
ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho.
Kaimu
Balozi huyo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Kanali Wilbert A.
Ibuge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katika
mazungumzo hayo, Katibu Mkuu ameeleza masikitiko yake kutokana na namna
ambavyo Ubalozi huo umekuwa ukitoa taarifa mbalimbali za ushauri wa
kiusafiri (travel advisory) zinazoandikwa na kusambazwa na Ubalozi wa
Marekani kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo suala la namna Tanzania
inavyoshughulikia ugonjwa wa COVID-19.
Akitolea
mfano Katibu Mkuu amezitaja taarifa zilizotolewa na Ubalozi huo siku
ya Jumatano 13 Mei, 2020 na ya siku ya Jumatatu 25 Mei, 2020 kwenye
mtandao wa “Twitter” wa Ubalozi huo ambazo zote
zilionekana kukusudiwa kutoa tahadhari kwa raia wa Marekani waliopo
nchini na wanaotarajia kuja Tanzania kuwa jiji la Dar es Salaam siyo
salama kutokana na kuwepo idadi kubwa ya wagojwa wa COVID-19.
Tahadhari
hizo pia zimeendelea kudai kuwa hospitali nyingi jijini Dar es Salaam
(bila ya kuzitaja hospitali hizo) zimefurika wagonjwa wa COVID-19 jambo
ambalo siyo kweli na linauwezekano wa kusababisha taharuki kwa
Watanzania na wageni kutoka nje ya nchi ilhali hali halisi sivyo ndivyo
inavyodaiwa.
Katibu
Mkuu amemjulisha Kaimu Balozi kuhusu umuhimu wa Ubalozi kutoa taarifa
zilizothibitishwa hususan kwa sababu serikali haina kizuizi cha aina
yoyote kwa Mabalozi kutafuta na kupata taarifa sahihi na zenye ukweli.
Katika
hatua nyingine, Katibu Mkuu amemshukuru Kaimu Balozi huyo kwa
ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Marekani
katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, biashara, uwekezaji, ulinzi
na usalama na maeneo mengine ya maendeleo.
Emmanuel Buhohela
MKURUGENZI KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI 26 MEI 2020
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akisalimiana na Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt mni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho.Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt mni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.
.Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt Imni Patterson akizungumza wakati alipokutana na Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Kanali Wilbert A. Ibuge. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za
Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimsikiliza Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt Imni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akisalimiana na Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt mni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho.Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt mni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimsikiliza Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt Imni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...