Na Leandra Gabriel, Michuzi TV


ANAFAHAMIKA zaidi kwa jina la "Mr.Ibu" ni John Ikechukwu Okafor mwigizaji na mchekeshaji kutoka nchini Nigeria, Okafor anatajwa kuwa mchekeshaji mashuhuri ndani na nje ya nchi hiyo anayemiliki utajiri mkubwa kupitia sanaa yake.

Okafor alizaliwa Oktoba 17, 1961 katika mji wa Enugu, Kusini Mashariki mwa Nigeria, alizaliwa na kukulia huko pamoja na kupata elimu yake ya msingi na sekondari pia an taaluma ya uandishi wa habari aliyoipata katika chuo cha (IMT.) Tangu akiwa shule Okafor alikuwa mbunifu hadi kufikia kiwango cha kuigiza, kutengeneza na kuongoza filamu mbalimbali nchini humo.

Ukuaji wa John Okafor ulikuwa na misukosuko mingi na hii ni kwa mujibu wake ambapo ameeleza moja ya vyombo vya habari nchini humo kuwa alikulia katika mazingira yenye changamoto na hiyo ni kutokana na hali duni ya familia yake ambayo ilikua moja ya familia dunia katika mji wa Enugu lakini hilo halikumzuia alipambana ili aweze kutoka kwenye dimbwi la umaskini.

Mr. Ibu alianza maisha kwa kuuza kuni baadaye akawa kinyozi na kuuza nyama katika mabucha shughuli ambazo zilimsaidia kuitunza familia yake.

Fani ya uigizaji aliinzia akiwa Sekondari na hakufikiri kama angeweza kuchekesha watu, na akaishia elimu ya sekondari kwa kuwa hakuwa na mtu wa kumsomesha zaidi.

Alijiunga na kiwanda cha filamu nchini humo (Noolywood) mwaka 1978 ambapo alisafiri kutoka Enugu hadi Nigeria kwa ajili ya kufanya sahili mbalimbali ambapo awali hakukubalika kwa kile alichoeleza kuwa hakuwa na mvuto.

Filamu ya Mr Ibu ya mwaka 2004 ndio iliyompa jina katika tasnia hiyo na mwaka 2005 alivunja rekodi kupitia filamu waliyoshirikiana na muigizaji Osita Iheme (Pawpaw)ambapo alitunukiwa tuzo ya mchekeshaji bora zaidi nchini Nigeria.

Okafor ameigiza filamu zipatazo 300 ikiwemo Mr Ibu in London, Mr Ibu, Ibu in Prison na Police Recruit huku akitajwa kuwa moja ya waigizaji wenye fedha nyingi nchini humo akiwa amepewa tuzo mbalimbali kwa miaka mingi mfululizo.

Katika kupambana na maisha Okafor amekumbana matukio mengi ya kusikitisha ikiwemo kupoteza wanafamilia 6 akiwemo baba waliokufa kwa sumu.

Mr. Ibu amebarikiwa mke (Stella Maris) na watoto watatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...