Na Amiri Kilagalila, Njombe.
Edwin Swale aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa
Njombe,ameshinda kura za maoni katika mkutano mkuu wa jimbo la Lupembe
mkoani Njombe kwa kupata kura 138 kati ya kura 421 kuwa mgombea wa
ubunge Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM huku Jorum Hongoli
aliyekuwa akitetea nafasi yake akipata kura 61.
Edwin Enosy Swale (wakili) alihamia Chama cha Mapinduzi Octoba 2019.
Mkutano wa kura za maoni umefanyika mapema hii Leo katika
ukumbi wa Turbo mjini Njombe kwa kuwapigia kura wagombea 19
waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...