KATIBU wa CCM Mkoa wa Tanga Shaibu Akwilombe akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza kuu la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Nassoro Makau.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Nassoro Makau akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Shaibu Akwilombe
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba akizungumza kushoto
ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Shaibu Akwilombe na kulia ni Katibu wa
CCM wilaya ya Tanga
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa kikao hicho
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa na Mwenyekiti wa Kamati
ya Utekelezaji ya UWT wilaya ya Tanga Sussan Uhinga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha moja na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Nassoro Makau na
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Tanga Moza Shilingi
wakiwa kwenye ;picha ya pamoja
BARAZA kuu la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga limempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa uongozi bora wenye uweledi na kusimamia maadili kwa watumishi wa umma huku wakieleza kwamba anastahili kuendelea kuwatumikia watanzania.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Nassoro Makamu alisema kwamba Rais Magufuli amefanya kazi kubwa iliyotukuka ya kuhakikisha anawapa maendeleo watanzania hivyo wataendelea kumuunga mkono kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Alisema kwamba tarehe 14 ndio siku ya kuchukua fomu ua kuwania nafasi za udiwani na Ubunge na baadae uchaguzi huu lengo la chama na nia ya dhati kwa kauli ya wazazi ni kumuhakikishia kura nyingi Rais Magufuli kwa mkoa wa Tanga kwa asilimia 98 .
Alisema kwani wao kama wazazi ni jeshi kubwa kwa sababu katika jumuiya hii vijana wapo, uwt wapo hivyo hawana sababu ya kuacha kumpa kura zote Rais Dkt Magufuli kwa wakati wa uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyikamwezi Octoba mwaka huu.
“Ndugu zangu tunakwenda kwenye uchaguzi sisi kama wazazi tuhakikisha tunampa kura za ndio Rais Dkt Magufuli kwa asilimia 98 huku 78 zikitoka kwa wazazi na hatutashindwa kufanya hivyo kwa sababu wazazi ndio wenye kutafsiri elimu ya malezi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020”Alisema
Awali akizungumza wakati akifungua mkutano huo Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Akwilombe aliwataka kwenda kuitafsiri dhana ya elimu ya malezi kuelekea kwenye uchaguzi mkuu maana ya moja ya mambo yanayowapa changamoto ndani ya chama ni ukosefu wa elimu ya siasa na elimu ya utambuzi. “Tatizo lenu kubwa ni kuitafsiri dhana ya elimu na malezi kwa mujibu wa wakati… kuna jambo ambalo linazungumzwa sana ni uchaguzi tukiwa kwenye maandalizi ya mchakato ndani ya chama hivyo niwaombe muitafsiri dhana ya elimu na malezi kuelekea kwenyue uchaguzi mkuu “Alisema
Alisema kwa maana moja ya mambo yanayowapa changamoto ndani ya chama ni ukosefu wa elimu ya siasa na elimu utambuzi kwa kuwa jumuiya ndio ina dhamana ya kusimamia masuala ya elimu na malezi naomba jumuia ya wazazi Tanga mjini muitafisiri dhana ya elimu na malezi wakati chama kikielekea kwenye uchaguzi mkuu wa nchi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...