Maafisa kutoka Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi ya Elimu ya Juu (HESLB) wakizungumza na Mwalimu Mkuu wa Shule
ya Sekondari Geita, Isaya Busagwe (katikati) wakati walipofika shuleni
hapo kutoa elimu kuhusu mwongozo wa utoaji mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu
ya Juu kwa mwaka 2020/2021 yaliyoendeshwa na HESLB kwa wanafunzi
waliohitimu masomo ya kidato cha Sita na Stashahada Mkoani Geita.
Mafunzo hayo yalifanyika jana Jumatatu (Julai 27, 2020). Kushoto ni
Meneja wa HESLB Kanda ya Ziwa, Ussama Choka.

Wanafunzi wa Kidato cha Sita
katika Shule ya Sekondari ya Kilangalala iliyopo Mkoani Geita wakinawa
maji kwa kutumia vitakasa mikono muda mfupi kabla ya utoaji elimu kwa
umma kuhusu mwongozo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu kwa
mwaka 2020/2021 kwa mwaka 2020/2021 yaliyoendeshwa na Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa wanafunzi waliohitimu masomo ya
kidato cha Sita na Stashahada yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari
Geita Mkoani Geita jana Jumatatu

Afisa Elimu (Taaluma) Mkoa wa
Geita, Kaitila Mafwimbo akizungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari
za Kalangalala na Geita pamoja na waliohitimu masomo hayo wakati utoaji
elimu kuhusu mwongozo wa utoaji mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa
mwaka 2020/2021 yaliyoendeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
(HESLB) kwa wanafunzi waliohitimu na wanaondelea na masomo ya kidato cha
Sita na Stashahada Mkoani Geita. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika
Shule ya Sekondari Geita Mkoani Geita jana Jumatatu

Meneja Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Kanda ya Ziwa, Ussama Choka
akizungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari za Kalangalala na Geita
waliosoma kidato cha sita na wale waliohitimu masomo hayo wakati utoaji
wa elimu kuhusu mwongozo wa utoaji mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu
kwa wanafunzi waliohitimu na wanaondelea na masomo ya kidato cha Sita
pamoja na Stashahada. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Shule ya
Sekondari Geita Mkoani Geita

Baadhi ya wahitimu wa kidato cha
sita kutoka katika Shule mbalimbali Mkoani Geita wakifuatilia kwa makini
mafunzo ya elimu kwa umma kuhusu mwongozo wa utoaji mwa wanafunzi wa
Elimu ya Juu kwa mwaka 2020/2021 kwa wanafunzi waliohitimu na
wanaondelea na masomo ya kidato cha Sita pamoja na Stashahada
yaliyotolewa na Maafisa kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi ya Elimu ya
Juu (HESLB). Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Geita
Mkoani Geita
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...