NA ANDRRW CHALE

Mwanamama Bona Kamoli  ameongoza katika kura za maoni zilizopigwa leo  Julai 20 Jimbo la Segerea.

Katika zoezi hilo Wajumbe 525 wameweza kuwapigia kura wagombea 95 waliojitokeza katika zoezi hilo.

Katika matokeo hayo, kura Nne ziliharibika huku baadhi ya wagombea wakipata sifuri kutokana na  kutojipigia huku wagombea wengine wakiambulia kura moja.

Miongoni mwa watia nia hao ni pamoja na Mwandishi wa Habari wa Clouds  Media, Antonio Nuga ambaye pia Msemaji wa Yanga aliyeambulia kura 1 huku Msanii mkongwe Hashim Kambi nae akiambulia kura moja.

Matokeo ya kura za Maoni:
1. Bona Kamoli kura 374
2. Asaa Simba kura 41
3. Shaban Oronu kura 20
4. Daniel Mwakajumbiki kura 17
5. John  Ryoba kura 9
6. Baraka Omary kura 9

Zoezi hilo la matokeo yametangazwa na Katibu wa CCM Wilaya, Iddi Mkoa.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...