Na Amiri Kilgalila,Njombe Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoa wa Njombe Rose Mayemba,amesema chama hicho kimejipanga kuweka wagombea wa ubunge katika majimbo yote ya uchaguzi mkoani Njombe
Rose ameyasema hayo mkoani Njombe mapema hii leo wakati wa mahojiano na kituo cha Radio King’s kilichopo halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo
“Wananchi wajitokeze kuwasikiliza pale ambapo tutakuwa tumeanza mtanange,tunawagombea katika majimbo yetu yote sita na ni wagombea wazuru tunaamini mambo yatakuwa mazuri” Rose Mayemba Mwenyekiti Chadema Njombe
Vile vile Rose amesema “Chadema mkoa wa Njombe tumejiandaa na tunawagombea wa kutosha,tuna kata 107 lakini tunawagombea karibu kila na ni mkakati kwamba hakuna kata itakwenda kwenye uchaguzi bila kuwa na mgombea” Rose Mayemba Mwenyekiti Chadema Njombe
Mkoa wa Njombe una jumla ya majimbo 6 ya uchaguzi likiwemo jimbo la Njombe mjini,Makambako,jimbo la Ludewa,Makete,jimbo la Lupembe pamoja na jimbo la Wanging’ombe yote yakiongozwa na Chama cha mapinduzi CCM.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...