Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema amesikitishwa na kifo cha Rais mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa huku akieleza kuwa jana Julai 23, 2020 alikwenda kumuona hospitali na wala hakuwa na hali mbaya kiasi cha kutia shaka.

Akizungumza leo Julai 24, 2020 nyumbani kwa Mzee Mkapa Masaki jijini Dar es salaam,  Dk.Kikwete ambaye aliachiwa kijiti cha Urais na Mkapa , amesema "Sijui nianze wapi....Unajua kifo ni siri ya Mungu. Jana nilikwenda kumuona hospitali.

"Tulizungumza sana. Kwa kweli tulizungumza sana, alikuwa na maumivu lakini sio yale ukitoka kumuangalia mgonjwa unawaambia wenzako nimemuona lakini...Alikuwa na maumivu ya kawaida. Tumezungumza kwa zaidi ya lisaa limoja. Tulizungumza mambo mengi . NA ule usiku wa manane nilipopata taarifa KWAMBA mzee kule amefariki, nikauliza imetokea nini tena kwa sababu hakuwa katika hali mbaya kiasi hicho.

"Nilikwenda muona na kisha kumuaga kwamba nitakuja tena kesho (leo Julai 24) lakini itakuwa vizuri nikija nikukute umetoka hospitali, uwe nyumban. Hata kusema kwamba tumeagana kabisa, suala kubwa tumepoteza moja ya viongozi mashuhuri , viongozi wa kuu wa nchi yetu.

"Mtu ambaye amelitumikia Taifa letu kwa heshima kubwa kwa uadilifu mkubwa na kwa moyo na moyo wa upendo. Lakuomba tu kwa watanzania katika kipindi hiki ni kuendelea kuomboleza. 

"Kuwa na moyo wa uvumilivu, kukubali kifo kimeumbwa na Mungu na kila mmoja ndio njia yake.Waislam tunasema sote ni waja wake na kwake tutarejea, sasa tutarejea lini ni siri yake aliyetuleta duniani,"amesema Dk.Kikwete.

Hata hivyo amesema mzee Mkapa amefanya mambo mengi, hivyo yale ambayo ameyasimamia yaendelezwe kwa maslahi ya Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...