Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, SACP- Lazaro Mambosasa akiwaonesha waandishi wa habari namba za gari T 832 DCW ambazo ndiyo namba halisi za usajili wa gari.
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, SACP- Lazaro Mambosasa akiwaonesha waandishi wa habari kofia iliyokamatwa kwenye gari la magambazi.
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, SACP- Lazaro Mambosasa akiwaonesha waandishi wa habari pingu zilizokamatwa.
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewaua majambazi watatu na
kukamata silaha mbili aina ya Short Gun Pump Action na Bastola aina ya
Browning.
Mnamo
tarehe 26.07.2020 majira ya saa mbili usiku
Jeshi la Polisi Kanda Maalum lilipata taarifa kuwa huko maeneo ya
Mbagala Chamanzi kuna gari lenye namba T
855 ATE aina ya Nissan X-Trail likiwa na watu wanne wanaosadikiwa
kuwa ni majambazi wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu.
Baada
ya kupata taarifa hizo kikosi kazi cha kupambana na ujambazi kiliweka mtego katika eneo hilo na baada majambazi hao kuhisi wanafuatiliwa na Polisi
ghafla walianza kupiga risasi hovyo kwa hofu na ndipo
askari wakaamua kujibu mapigo kwa kulishambulia gari la majambazi hao na kufanikiwa kuwaua papo hapo majambazi watatu na jambazi
mmoja akafanikiwa kukimbia.
Askari
walifanya upekuzi ndani ya gari la majambazi hao na kumkuta jambazi mmoja akiwa
amevalia mavazi ya Jeshi la Polisi aina ya kombati za kijani (JUNGLE GREEN) na kofia aina ya bareti
nyeusi ya Jeshi la Polisi, redio Call, Pingu, namba za gari T 832 DCW ambazo ndiyo namba halisi za
usajili wa gari hilo na silaha mbili aina ya Short gun Pump Action ikiwa na
risasi nne ndani ya magazine iliyofutwa namba na Bastola aina ya Browning
iliyofutwa namba ikiwa na risasi nne ndani ya Magazine.
Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa majambazi hao walifanya matukio ya uhalifu Mkoa wa
Pwani Wilaya ya Mkuranga maeneo ya Vikindu na Kisemvule ambapo mnamo tarehe
25/07/2020 majira ya saa mbili usiku
majambazi hao walimteka na kumpora
mfanyabiashara wa UWAKALA wa Benki na Mitandao ya simu aliyefahamika kwa jina
la SALEHE MASOUD kiasi cha Tsh 19,600,000/= .
POLISI
KANDA MAALUM KUIMARISHA ULINZI SIKUKUU YA EID EL-HAJJI.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum kwa kushirikiana
na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kikamilifu kuimarisha
ulinzi na usalama katika kipindi cha sikukuu ya Eid El-Hajji inayotarajiwa
kuadhimishwa tarehe 31/07/2020.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawaasa wananchi wa Jiji la Dar es
Salaam kusherehekea sikukuu kwa amani na
utulivu na kujiepusha na vitendo vya
uvunjifu wa sheria kwani tumejipanga kuimarisha doria maeneo yote muhimu
zikiwemo nyumba za Ibada, fukwe za bahari na tunawatadharisha watembea kwa
miguu na madereva wa vyombo vya moto kuendelea kufuata sheria za usalama
barabarani.
Aidha
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawaomba Wananchi wa Dar es Salaam
kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu kwani jukumu la kuzuia uhalifu ni la kila
Mtanzania.
SACP-
LAZARO B. MAMBOSASA,
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR
ES SALAAM.
30/07/2020.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...