Na Khadija Seif,Michuzi TV

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva Juma Jux ametoa pongezi kwa mwanamuziki nyota nchini Tanzania Nassib Abdull maarufu Diamond Platnum kwa kukipa nafasi ya kipeke kipaji cha mwanadada Zuchu ambaye ameingia kwa kasi katika ulimwengu wa muziki huo.

Jux ambaye amejipatia umaarufu kupitia staili yake ya kuimba muziki wa R&B amempongeza Diamond wakati wa hafla  ya utambulisho wa Zuchu iliyopewa jina Am Zuchu  Asante Nashukuru iliyofanyika Mliman City jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

"Zuchu yupo sehemu sahihi, natambua uwezo wa lebo ya wasafi (WCB) inayoongozwa na  Diamond platinum.Kipaji  chake kitafika mbali kutokana na mwanzo wake kuwa mzuri.Diamond amekipa nafasi kipaji cha Zuchu, nasi tutamsapoti,"

Kuhusu harakati zake za muziki, Jux alikuwa ana mpango wa kutoa Album yake ya pili lakini kutokana na kuvutiwa na sauti ya Zuchu ameamua kughairisha ili aweze kumshirikisha kwenye wimbo kwenye album hiyo.

"Nimevutiwa na sauti yake pamoja na uwezo wake wa kutumbuiza, hivyo nimeshawishika awepo kwenye album yangu hiyo mpya".
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...