Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akikabidhiwa Nyaraka za ofisi
kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.
Adolf Mkenda ikiwa ni makabidhiano rasmi ya ofisi yaliyofanyika katika
ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii zilizopo Mtumba Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akisaini kitabu cha makabidhiano
pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.
Adolf Mkenda (kulia) kwenye ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii
Mtumba Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akitoa neno kwa aliyekua Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda kwenye Kikao
cha Menejimenti Kilichofanyika mapema leo kwenye ofisi za Wizara ya
Maliasili na Utalii zilizopo Mtumba Jijini Dodoma

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda akiwashukuru viongozi wa Wizara
ya Maliasili na Utalii pamoja na watumishi wote wa Wizara ya Maliasili
na Utalii kwa ushirikiano waliompa wakati wa uongozi wake wakati wa
Kikao cha Menejimenti kilichofanyika kwenye ofisi ya Wizara ya Maliasili
na Utalii Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki akiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda pamoja
na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii mara
baada ya Prof. Adolf Mkenda kuaga watumishi wa Wizara ya Maliasili na
Utalii kwenye kikao cha Menejimenti kilichofanyika kwenye ofisi za
Wizara ya Maliasili zilizopo Mtumba Jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...