Na.Vero Ignatus.
Mwandishi wa habari Nguli Kisiwani Pemba Kawthar Iss-hack amechukuwa fomu ya kinyanga'anyiro cha viti maalum Ubunge UWT Mkoa wa Kusini Pemba leo
Kawthar ni mmoja kati ya Waongoza shughuli mbali mbali za Chama na Serikali za kitaifa na Kimataifa Visiwani Unguja na Pemba ambapo anatoka Idara ya habari Maelezo ofisi za Pemba.
Akizungumza Mara baada ya kuchukua fomu amesema kuwa pamoja na changamoto zinazowakabili wanawake wa Kusini Pemba amesema zinahitaji ushirikiano wa pamoja na kiongozi ambae atakuwa na ubunifu na mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa kinachofanyika katika mkoa huo ni kile kinachofanyika kwaajili ya ushirikishwaji wawanawake wenyewe.
Amesema wanawake wapewe nafasi ya kutoa mawazo ya Jambo ambalo wanalolihitaji wao ili liwawezeze kupiga hatua katika kufika mahali pale wanapohitaji kufika, kwaajili ya Maendeleo ya jamii nzima kwani changamoto ni nyingi Mambo ni mengi Ila yote yanahitaji nguvu za pamoja.
"Kwa Sasa Zile siasa za kudanganyana na kurubuni watu hazipo zimepitwa na wakati,kwani sisa za Sasa Ni zile za wazi zenye tija katika jamii"alisema Kawthar.
Amesema katika mkoa wa Kusini Pemba wanawake wafikie mahali waone kwamba hakuna haja ya kununuliwa kwa siasa badala yake wachague kiongozi atakayeweza kuwajibika na kuitumikia jamii na kuleta mabadiliko chanya na mapinduzi ya fikra.
Kisiwa cha Pemba chenyewe ni fursa hivyo wanawake wa Mkoa wa kusini hawana bidi kuzichangamkia fursa hizo kwa mali asili na malighafi ambazo zinapatikana kisiwani humo kwa kuwaongoza kipato na kupambana na changamoto ya umasikini miongoni mwa wanawake.
Vingenevyo watajikuta wakiona wanawake wa Mkoa mengine Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ikipiga hatua huku wao wakiwaacha viongozi wenye sifa za kuwaangunisha wao na wafadhili, kuwaunganisha na serikali na mihimili mengine muhimu ya kushirikiana nayo kwa lengo la maslahi wanawake wote wa Mkoa wa huo.
Pichani Ni Mwandishi wa habari Nguli Kisiwani Pemba Kawthar Iss-hack Mara baada ya kuchukua fomu ya kuwaniakinyanga'anyiro cha viti maalum Ubunge UWT Mkoa wa Kusini Pemba leo



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...