Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewapongeza na kuwashukuru wanahabari na wasanii wote nchini kwa uzalendo waliouonesha katika kipindi chote cha maombolezo ya kitaifa ya Hayati Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye alizikwa kijijini kwake Lupaso, Masasi jana.

Akitoa tathmini yake kuhusu maombolezo hayo ya kitaifa mjini Lindi leo, Dkt. Mwakyembe amesema kazi walizofanya wanahabari na wasanii kuelezea wasifu wa marehemu, mchango wake kitaifa na kimataifa kwa njia ya makala, vipindi maalum, mahojiano mbalimbali na tungo za kufariji, kuliwaza na kupeana moyo, zimeyabeba maombolezo yetu ya kitaifa.

“nimefurahishwa sana na kujitoa kwenu kwa hakika mmeonesha uzalendo wa juu sana kwa taifa letu ,naomba muendelee na moyo huo huo ili kuwa na taifa lenye wasanii na waandishi wa habari wenye umoja: Dkt. Mwakyembe

Aidha Dkt. Mwakyembe alizidi kufafanua kuwa kwa hakika wasanii na wanahabari wametekeleza jukumu walilokuwa nalo bila kuelekezwa, kusukumwa wala kusimamiwa bali kwa kujituma na kusukumwa na dhamira ya utaifa na uzalendo.

“Ndiyo maana katika hotuba zake zote kuhusiana na msiba huu, Mheshimiwa Rais hajaacha kutambua mchango mkubwa wa wanahabari na wasanii katika kuliunganisha Taifa kipindi hiki kigumu cha majonzi ,hongereni sna wasanii na wanahabari tembeeni kifua mbele, mmetekeleza wajibu wenu kikamilifu kama Watanzania” alisema Dkt. Mwakyembe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...