Wagombea ubunge jimbo la Arumeru magharibi wskisubiri matokeo katika kura za maoni kwenye Mkutano mkuu wa wajumbe wa ccm wa halmashauri kuu ya Wilaya ya Arumeru magharibi Mkoani Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Hai,Mkoani Kilimanjaro ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Arusha Magharibi Lengai Ole Sabaya akipiga kura katika mkutano huo.
Msimamizi wa uchaguzi wa kura za maoni Naftali Joseph Robert akitangaza matokeo ya wagombea walioshiriki mchakato wa kura za maoni kwa wanachama wanaoomba kuteuliwa kugombea ubunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Mkoani Arusha.

=====   =====   ========

Na,Jusline Marco;Arusha

MKUTANO Mkuu wa Chama Cha Mapindizi(CCM Wilaya wa Uchaguzi wa kura za maoni kwa wanachama wanaoomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi umefanyila leo ambao Noel Severa ameibuka kidedea kwenye kua hizo kwa kupata 113 akifuatiwa na Joseph Lukimai aliyepata 66.

Akitangaza matokeo hayo leo katika mkutano huo uliofanyika jijini Arusha msimamizi wa uchaguzi juo Naftali Joseph Robert amesema kuwa nafasi ya tatu imeshikwa na David Sigala aliyepata kura 59 kati ya wajumbe 611.

Aidha katika matokeo hayo Furaha Lekoko alipata kura 54 alifuatiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha ambaye alipata kura 44 huku wakatiAmina Mollel aliyekuwa mbunge wa viti maalum walemavu akipata kura 41.

Kwa upande wa Katibu wa CCM wilaya ya halmashauri ya Arusha Hamisa Chacha amewataka wagombea na wajumbe kuache tabia ya kusheherekea matokeo ya kura za maoni bali wasubiri na kutoa nafasi kwa vikao vya uteuzi kufanya kazi yake ya uteuzi wa wagombea hao.

"Pamoja na kuwepo kwa uwazi katika zoezi hilo wagombea wafahamu kuwa ushindi huo siyo kigezo cha kukufanya wewe uteuliwe bali ni hatua za awali katika chakato mzima wa kugombea nafasi ya ubunge."alisisitiza katibu huyo.

Mwenyekiti wa wilaya hiyo Saimon Saning'o alisema kuwa ni vyema wagombea wote waendelee kupendana na mshindi katika uteuzi huo asinyanyue mabega kwa wenzie kwani mayokeo hayo siyo mwisho wa maamuzi hivyo wasubiri jina litakalorudishwa na halmashauri kuu.

Aidha katika mkutamo huo watia nia wawili ambao ni Zakaria John Mpala na Dkt.Nimrod Sigala hawakuweza kujitokeza katika kuomba kura za kuwania nafasi hiyo ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi ambapo msimamizi wa uchaguzi huo aliomba kura kwa niaba yao.

Nao baadhi ya watia nia waliweza kujinadi kwa sera mbalimbali huku vipaumbele vikuu walivyoahidi kuanza navyo endapo watapatiwa ridhaa ya kuwa wabunge ni kushughulikia kero mbalimbali na kuzitatua ikiwelo miundombinu ya barabara na umeme,elimu,afya na maji.

Katika mkutano huo wagombea wa ubunge jimbo la Arumeru Magharibi walikuwa 61,jimbo la Arumeru Mashariki 33,Jimbo la Arusha mjini ikiwa 92 ambapo mgombea mmoja halurudisha fomu huku Jimbo la Monduli wakiwa 24,Longido 12 na Ngorongoro 14.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...