Balozi
wa Denmark nchini Mhe. Mette Dissing-Spandet akisaini kitabu cha
maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa leo
tarehe 26 Julai 2020 jijini Dar es Salaam
Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa 


Baadhi ya mabalozi wakiwa
katika picha ya pamoja na mama Anna Mkapa mara baada ya kutoa salamu za
pole nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa Ubalozi wa Uganda nchini Bibi. Musekura Eseza akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa.
Mwakilishi
wa Ubalozi wa Sweden nchini Bw. Michael Sulusi akisaini kitabu cha
maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa
Mwakilishi wa Ubalozi wa Sudan nchini Bw. Jaafar Nasir Abdalla akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
Mwakilishi wa Ubalozi wa Uturuki nchini Bw. Onur Yay akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
Balozi
wa Hispania nchini Mhe. Fransisca Pedros akisaini kitabu cha maombolezo
nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa leo tarehe 26
Julai 2020 jijini Dar es Salaam






Balozi wa Morocco nchini Mhe. Abdelilah Benryane akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
Balozi wa Zambia nchini Mhe. Benson Keith Chali akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
Balozi wa Congo DRC nchini Mhe. Jean -Pierre Mutamba akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa



Balozi wa Somalia nchini Mhe. Mohamed Hassan akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
***********************************
Mabalozi mbalimbali
wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, wameendelea kujitokeza kusaini
kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin
Mkapa na kumuelezea kuwa ni kiongozi mahiri na msuluhishi nguli wa amani
barani Afrika na duniani.
Mara baada ya kusaini kitabu
cha maombolezo, baadhi ya mabalozi hao wakaelezea walivyoguswa na msiba
wa Mkapa na kusema Tanzania imepoteza kiongozi na msuluhishi nguli wa
amani barani Afrika na duniani.
Kwa upande wake, Balozi wa
Zambia nchini Mhe. Benson Keith Chali amesema kuwa Zambia wameguswa sana
na msiba kwani Tanzania na Zambia ni ndugu, “toka mwanzoni Nyerere na
Kaunda walikuwa ndugu na sisi tumeendelea kuwa ndugu na unapopoteza
ndugu unaumia sana. Sisi kama Zambia kwa kweli tumepokea kwa masikitiko
makubwa tarifa za kifo cha Mzee Mkapa,” .
“Tutamkumbuka Mzee Mkapa kama
kiongozi aliyesimamia amani maeneo mbalimbali barani Afrika ikiwemo
Kenya, Burundi, Congo DRC, na kwingineko duniani,” amesema Mhe. Keith
Chali
Mhe. Keith Chali ameendelea
kusema kuwa “Sisi kama Zambia tunatoa sana pole kwa familia yake,
Serikali ya Tanzania na Watanzania kwa ujumla ……tunaomboleza wote msiba
huu mzito,”.
Nae Balozi wa Denmark nchini
Mhe. Mette Dissing-Spandet amesema kuwa Rais Mstaafu Mzee Mkapa alikuwa
kiongozi mahiri kwa Tanzania lakini pia alikuwa rafiki na mfano wa
kuigwa na mataifa mbalimbali.
“kwetu sisi kama Denmark alikuwa rafiki na tutaendelea kumkumbuka daima kwa upendo wake,” Amesema Mhe. Mette.
Aidha, nae Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal amesema
kuwa Mzee Mkapa alikuwa mtetezi wa amani barani Afrika na atakumbukwa
kwa mema aliyoyafanya kwani aliyafanya kwa jitihada na weledi wa hali ya
juu, Mungu ampumzise kwa Amani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...