Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MAKAMU wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amesema kinachoendelea sasa ni hadithi ya Paukwa pakawa huku akifafanua akiondoa mtu,anakaa mtu na kazi ya kuendelea kuwatumia Watanzania inaendelea.

Mama Samia ameyasema hayo leo Julai 20,mwaka 2020 Ikulu ya Chamwino Mjini Dodoma baada ya viongozi walioteuliwa kushika nafasi mbalimbali kuapishwa kutokana na wale waliokuwa wakishika nafasi hizo kuomba ruhusa kwa Rais Dk.John Magufuli kwenda kuwania nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu.
"Kinachoendelea sasa ni hadithi ya Paukwa pakawa, kaondoka mtu, anakaa mtu kuendelea kazi ya maendeleo ambayo inafanyika kwa kasi kubwa.Kama kasi umeikuta ndogo hakikisha unaiongeza, wateule wote naamini mtakwenda kutekeleza majukumu yenu ya kuwatumikia watanzania kwa kasi inayokwenda nayo Serikali.
"Wateule wote ambao mmeapishwa leo hii nendeni mkachape kazi.Watanzania wanaimani kubwa na ninyi ambao mmepata fursa hii kati ya wengine wengi,"amesema Mama Samia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...