Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Dk.Sophia Mejama amesem kuna habari za upotoshaji ambazo zimekuwa zikisambazwa kwamba anaenda kugombea Ubunge Jimbo la Mwanga na Mama Anna Kilango.

Dk.Mjema kupitia taarifa yake aliyoitoa leo Julai 3,2020 kwa vyombo vya habari amesema kwamba huo ni uongo na uzushi na si taarifa za kweli. " Afadhali mtakayokua mnayaona au kusikia niulizeni mwenyewe na nitawapa ushirikiano. 

"Mimi sitoki jimbo la Mwanga, bado nipo sana hapa Ilala na  kipindi hiki mtasikia mengi, tafadhali yapuuzeni. Bado naendelea kuitekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kumsaidia kazi Rais wetu Jemedari Dk.John Pombe Joseph Magufuli,"amesema Dk.Mjema.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa atachukua hatua dhidi ya upotoshaji huo dhidi yake kwani baada huo uzushi kusambaa umeleta taharuki kwake na kwa watu wengine,hivyo hilo ni kosa kama makosa mengine."Tuendelee kuchapa kazi, kwa maendeleo ya Ilala yetu.  CCM Oyeeeee"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...