Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
RAIS
Wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameitisha kikao cha dharura kufuatia
mtu mmoja anayeshukiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid
-19) kuingia nchini humo kwa kuvuka mpaka kinyemela akitokea Korea
kusini, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti tukio hilo leo.
Imeelezwa kuwa kisa hicho kinakuwa cha kwanza kuripotiwa nchini humo na tayari mshukiwa amefanyiwa vipimo na amewekwa karantini.
Kim ametangaza hali ya dharura nchini humo na kuagiza kuweka vizuizi katika mpaka kwenye mji wa Kaesong kwa tahadhari zaidi.
Imeripotiwa
kuwa mshukiwa huyo alikuwa Korea kusini kwa miaka mitatu na alirejea
nchini humo Julai 19 mwaka huu kupitia mpaka unaotenganisha nchi hizo
mbili kabla ya kukutwa na dalili za Covid-19.
Korea
Kaskazini imepokea maelefu ya vipimo vya Corona kutoka Urusi na mataifa
mengine na ilifanikiwa kuweka vizuizi hasa mipakani lakini baadaye
masharti hayo yakalegezwa.
Aidha
Kim ameagiza uchunguzi kwa vyombo vya ulinzi katika mpaka ambao
mshukiwa huyo alipita na kuchukua hatua muhimu ikiwemo adhabu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...