Muhammed Khamis,TAMWA-Zanzibar.
WATENDAJI wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake TAMWA-Zanzibar  wamekutana na kujadili utendaji kazi wa shughuli mbali mbali kwa Chama  hicho kwa muda wa miezi sita kutoka mwezi Januari hadi Juni mwaka huu.

Mkutano huo wa siku mbili ulifanyika  katika ukumni wa chama hicho
uliopo Tunguu wilaya ya kati Unguja ambapo pia umewakutanisha watendaji  kutoka ofisi za Pemba.

Awali Mkurugenzi wa Chama hicho Zanzibar Dkt,Mzuri Issa amewataka
watendaji hao kuhakikisha wanaendeleza kufanya kazi zao kwa ufanisi
mkubwa.

Alisema ufanyaji kazi kwa bidii ndio nguzo kuu ya kuiasaidia jamii
katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba hususani haki za wanawake
na watoto.

Aliwataka wafanyakazi hao kufahamu kuwa jamii inakabiliwa na changamoto  mbali mbali hivyo wafanyakazi hao wanapaswa kutambua kuwa wana wajibu  mkubwa kwa jamii.

Miongoni mwa wafanyakazi hao walisema kufanyika kwa mkutano huo wa siku  mbili kutaongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi z akila siku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...