Na Abdullatif Yunus Michuzi Tv.
Semina Maalum Wezeshi kwa Wajasiriamali kufikia matakwa ya Viwango inayoratibiwa na Shirika la Viwango Nchini TBS imewafikia wajasiriamali wa Mkoa wa Geita na kuhudhuriwa na Washiriki ambao ni sehemu ya Wajasiriamali Mkoani humo.
Semina hiyo ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo mengine yaliyowahi kutolewa mapema mwaka huu, Ina lengo la kuwafanya Wazalishaji wa bidhaa hasa wajasiriamali wadogo, kujiinua na kufikia Matakwa ya Viwango ikiwa ni pamoja na namna gani bidhaa zao zitakubalika katika soko la ushindani.

Mgeni Rasmi katika Semina ya Mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Geita Ndg. Fadhili Mohammed amewasisitiza wajasiriamali hao kuongeza ubora wa bidhaa wanazozalisha, ili kuinua kipato chao jambo ambalo litawafanya wajasiriamali hao kujiinua kiuchumi mtu mmoja mmoja na Taifa kwa kwa ujumla, na kwamba Geita ya sasa tofauti na Mikoa mingine inatakiwa kusifika kupitia uzalishaji wa bidhaa zinazokidhi Viwango.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita, Fadhil Mohammed akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa Semina ya Mafunzo Maalum Wezeshi ya Wajasiriamali kufikia Matakwa ya Viwango Mkoani Geita Mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo katika Ukumbi wa SIDO.
Meneja
Mafunzo na Utafiti kutoka TBS, Hamisi Sudi Mwanasala akisoma hotuba
mbele ya Mgeni Rasmi na Washiriki wa Semina ya Mafunzo kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu TBS.
Mgeni
Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Fadhili Mohammed akisikiliza maelezo ya
namna bidhaa ya Mafuta inavyotengenezwa kutoka kwa miongoni mwa
wajasiriamali walioshiriki Semina ya Mafunzo Wezeshi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...