Na Tulizo Kilaga-TFS
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce k. Nzuki ameupongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa jinsi ulivyojiopanga kuonesha shughuli zake ikiwa ni pamoja na juhudi inazozifanya za kuelimisha jamii kuhusu uhifadhi wa misitu, uendekezaji utalii ikologia na wa Malikale.
Ametoa pongezi hizo leo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kuijonea shughuli mbalimbali zinazoendelea katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaliyoanza tarehe 01 - 13 Julai, 2020 katika viwanja vya Mwl. Nyerere.
Amesema ameridhishwa na namna TFS ilivyojipanga na jinsi walivyo mahiri katika kutoa maelezo kwa wananchi kuhusu shuguli zinazofanywa na taasisi hiyo na kuitaka menejimenti ya TFS kufanyia kazi mapendekezo yote aliyowahi kuyatoa kwa lengo la kuboresha utendaji wa taasisi hiyo.
“Nimefurahishwa kuona shuguli zote mnazofanya ziko bandani hapa, nimepata historia nzuri ya michoro ya Kondoa Irangi, Hifadhi za Mazingira Amani ziko hapa zikiwakilishwa na hifadhi mama Amani, lakini pia Kurugenzi ya uzalishaji mbegu za miti imeimarika na wanatoa mbegu na miche bora ya matunda na miti kwa wananchi,
“hakika mmejipanga hata nimeweza kuona jinsi mlivyojipanga kupambana na moto kupitia satalaiti ya kufuatilia Majanga ya moto, sasa nitowe wito kwa jamii kuungana na serikali kulinda na kuhifadhi misitu, Serikali inatimiza wajibu wake na jamii ishiriki kuhifadhi maliasili zilizopo nchini kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho,” alisema Dkt. Nzuki.
Naye, Kaimu Meneja wa Mawasiliano TFS, Martha Chassama amemshukuru naibu katibu mkuu kwa kutenga muda wake kutembelea na kutumia muda mwingi kwenye kila eneo la TFS lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii licha ya kuwa na majukumu mengine.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...