Na Shamimu Nyaki – WHUSM
Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza rasmi
kuwa kuanzia leo Julai 29, 2020  Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam utaitwa Uwanja wa
Uwanja wa Benjamin Mkapa (Benjamin Mkapa Stadium) ili kuendelea kumuenzi Rais huyo wa
awamu ya Tatu.

Rais Magufuli ametoa tamko hilo  katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa rais wa serikali ya
 awamu ya tatu Hayati Benjamin William Mkapa   iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru
Dar es Salaam  ambapo alisisitiza  Mzee Mkapa alikuwa na mchango mkubwa  katika sekta ya
michezo nchini hivyo taifa tunapaswa kumuenzi .

“Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo na alikua hapendi vitu viitwe kwa jina
lake,lakini kwakuwa kwa sasa amelala na hawezi kuniadhibu na kwakua nimepokea meseji
nyingi nimekubali na sasa natamka rasmi uwanja ule uitwe Mkapa Stadium,”Dkt.Magufuli.

Dkt.Magufuli ameongeza katika  Michezo  Mzee Mkapa alikuwa  anapenda sana michezo ndio
maana amefanya mambo mengi sana katika sekta hiyo,vile vile alikua ni Shabiki wa Timu ya
 Yanga japo hakuwahi kuonyesha hadharani hivyo tunapaswa kumkumbuka na kutunza
kumbukumbu   hizo.

Hata hivyo Uwanja wa Taifa Dar es Salaam (Mkapa Stadium) ni miongoni mwa viwanja
vikubwa barani Afrika ambavyo vimekidhi vigezo vyote vilivyoanishwa na Shirikisho la
Soka Duniani FIFA na una uwezo wa kuingiza mmashabiki takriban elfu sitini.

Hivi karibuni watu wengi walionyesha nia yao ya kuomba uwanja huo uitwe jina la
Mzee Mkapa kama njia ya kumuenzi Rais huyo mstaafu ambayo leo Mhe.Rais
 ameitimiza nia hiyo.

Pamoja Mheshimiwa Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa Mzee Mkapa katika sekta ya Sanaa
 napo ameacha alama kwani ndiye aliyeanzisha Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki  (COSOTA)
ambayo kwa sasa ni taasisi rasmi lengo ni kuwasaidia wasanii kupata haki za kazi zao na
 katika sekta ya Habari ndiye muasisi wa Vitengo vya Habari na Mawasiliano katika wizara.

Naye mmoja wa wananchi na shabiki wa mpira nchini Bw.Athuman Ugassa amepongeza uamuzi
Mheshimiwa Rais Magufuli wa kuupa uwanja huo jina lake kwani uwanja huo ni alama ya
mchango wake katika kuendeleza sekta  ya michezo nchini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...