Waziri Mkuu wake, Jenerali Alain Guilaume kulia akiwa na  waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasiri jijini Dar es Salaam.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SERIKALI ya Jamhuri ya Burundi kupitia Waziri Mkuu wake, Jenerali Alain Guilaume ambaye amemwakilisha Rais wa nchi hiyo na raia wote wa nchi yao wametoa pole kwa Watanzania kwa msiba mzito wa kuondokewa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa.

Akizungumza leo Julai 28,2020 Waziri Mkuu wa Burundi amesema amesimama hapo kwa niaba ya Rais wa Burundi na raia wote wa nchi hiyo kutoa salamu za pole kwa Watanzania.

"Ningependa kwanza kumshukuru baba Mungu kwa kutuwezesha kufika hapa, namshukuru Rais wa Tanzania na viongozi wote wa nchi nzuri
"Nimesimama hapa kumwakilisha Rais wa Burundi ambaye amenituma kuja hapa Tanzania katika nchi nzuri, nchi rafiki, nimekuja hapa nikiwa na viongozi kadhaa ambao nimeambatana nao.

Kwa niaba ya Rais wetu na kwa niaba ya Warundi wote tunatoa salamu za rambi rambi kwa msiba mkuu ambao Tanzania imepata.

"Salamu zetu ni kwamba Warundi wameungana na Rais wao kuungana nanyi, wanawapa pole, wanawafariji, Rais Dk.Magufuli, Rais wangu amenituma upokee pole na faraja, anakupa pole na kukufariji kwa msiba mkubwa.Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa mahali pema peponi , Amina."Amesema Guilaume

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...