Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene (MB) amesema Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuziba mianya ya uingizaji na usambazaji wa dawa za kulevya, usafirishaji wa binadamu na uhalifu unaovuka mipaka.

Waziri Simbachawene amesema hayo leo jijini Dodoma, wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa Wakuu Makao Makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi kilichofanyika kwa muda wa siku tatu, kikao ambacho kililenga kufanya tathimini ya utendaji wa kazi za Jeshi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa, Vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga imara kuhakikisha vinaimarisha hali ya usalama hususani kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu huku akiwataka wananchi pamoja na wanasiasa kutimiza wajibu wao kwa kutojiingiza kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene (MB) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...