TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Mkoani Manyara, inamshikilia mkazi wa Mjini Babati Yuda Sendeu akidaiwa
kuzuia shilingi milioni 44.7 fedha za chama cha kuweka na kukopa cha
Babati Saccos.
Mkuu wa
TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza mjini Babati
amesema Sendeu alichukua mkopo wa shilingi milioni 35 na kutakiwa
kurejesha shilingi milioni 44.7.
Makungu amesema Sendeu alichukua mkopo huo mwaka 2010 na alitakiwa kurudisha mkopo huo baada ya miezi 24 pamoja na riba.
Amesema
uchunguzi unaonyesha Sendeu alifanya makubaliano ya kihalifu na baadhi
ya wanachama wa Babati Saccos waliochukua fedha katika Saccos hiyo bila
kurejesha.
Amesema walifanya hivyo ili haki za wanachama waaminifu wa Saccos hiyo ziweze kupotea.
"Hadi
wanachama waaminifu wa Saccos hiyo wanafikisha malalamiko ya dhuluma
hiyo TAKUKURU Sendeu, bila kustahili amekaa na fedha hizo kwa miaka 10,"
amesema Makungu.
Ametoa
rai kwa wanachama wa Babati Saccos wanaofahamu kuwa wamechukua fedha za
Saccos hiyo na muda wa kurejesha umepita wafike kwa hiyari kwenye ofisi
za TAKUKURU.
Amesema
wanatakiwa wafike kwenye ofisi hizo Agosti 10 mwaka huu ili wapewe
hesabu zao na kuzirejesha na kwa wale watakaokaidi hatua kali dhidi yao
zitachukuliwa kuanzia Agosti 12 mwaka huu.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara Holle Joseph Makungu akizungumza na wandishi wa habari mjini Babati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...