Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MWANAMITINDO Wa kucha kutoka Houston, Texas Ayanna Williums ndiye mwanamke anayeshikilia rekodi ya mtu mwenye kucha ndefu zaidi ulimwenguni na tayari Guinness World Record imempatia tuzo mwaka 2018.
Ni kucha zilizofugwa kwa miaka 23 zikiwa na urefu wa sentimeta 18.
Mwanamtindo huyo ametumia miaka 23 kufuga kucha hizo na kuzipaka rangi kila wiki ili zionekane maridadi zaidi.
Akifanya mahojiano na vyombo vya habari huko Houston Ayanna alieleza kuwa amekuwa akikumbana na changamoto mbalimbali katika safari yake ya kufuga kucha hasa kutenga siku kwa kila juma kwa kupaka rangi pekee pamoja na kupata taabu kupandisha suruali alizovaa kutokana na urefu wa kucha zake.
"Nimekuwa nikitazamwa sana kucha zangu na kujiona wa tofauti sana licha ya familia na marafiki kuona ni kawaida" ameeleza Ayanna.
Kuhusiana na matunzo ya kucha zake Ayanna ameeleza kuwa anatumia sabuni mbalimbali za kuua vimelea na brashi za kucha na huzisafisha kila siku ili kuzipa nafasi ya kukua zaidi.
Wakati akipokea tuzo Ayanna alisema kuwa ni ndoto kupokea tuzo hiyo ya kimataifa na kueleza kuwa ili kufanikiwa jambo inahitajika nidhamu, uthubutu na subira.
Mwisho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...