Wataalam
wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakitoa huduma kwa
wananchi walioshiriki mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia
matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika taasisi
hiyo leo wakati wa mbio hizo zilizofanyika katika viwanja vya Farasi
Oyster bay Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi hundi ya
Shilingi milioni 200 iliyotolewa leo katika viwanja vya Farasi Oyster
bay Jijini Dar es Salaam na Benki ya CRDB zilizokusanywa kutoka kwa
washiriki wa mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia matibabu ya
watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Prof. Mohamed Janabi tuzo iliyotolewa leo katika viwanja vya Farasi
Oyster bay Jijini Dar es Salaam na Benki ya CRDB kutambua huduma
zinazofanywa na taasisi hiyo wakati wa mbio za CRDB Marathon kwa ajili
ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI.
Wafanyakazi
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walioshiriki mbio za CRDB
Marathon kwa ajili ya kuchangia watoto wenye magonjwa ya moyo
wanaotibiwa katika taasisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya
kumaliza mbio hizo zilizofanyika katika viwanja vya Farasi Oyster bay
leo Jijini Dar es Salaam



Picha na JKCI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...