Meneja uzalishaji wa kiwanda pekee Afrika cha kutengeneza viuadudu kilichopo kibaha mkoani pwani Gaspa Kimbi akielezea namna dawa hiyo inavyotengenezwa faida zake na haina madhara kwa binadamu inaweza kuwekwa kwenye majinya kunywa ambayo hayajafunikwa
 

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani imekiri kupingua kwa wagonjwa wa Malaria kutokakana na kutumia dawa ya kuulia viluilui vya mbu inayotengenezwa na Kiwanda cha Serikali cha kutengeneza dawa ya viuwadudu kilichopo Mjini hapa Mkoa wa Pwani

Akizungumza leo Agosti 7,2020, Mratibu wa Malaria katika Halmashauri hiyo Ally Shaha amesema tangu wakazi wa mji huo waanze kutumia dawa hiyo kiwango cha wagonjwa wa Malaria kimepungua kutoka asilimia 10 ya mwaka 2014 na 2015 hadi asilimia 2016 -2017 ambapo kilielezwa ni asilimia 0.8 .

Shaha amesema, kuanziehwa kwa kiwanda hicho imekuwa mkombozi kwa wananchi waliokuwa wanataabika na ugonjwa wa malaria.

Mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Tangini Joyce Michael amesema utumiaji wa dawa ya kuulia viluilui vya mazalia ya mbu imesaidia kutokomeza Malaria katika familia yake na jamii inayomzunguka

Nurdin Mayoyo mkazi wa Uyaoni Halmashauri ya mji wa Kibaha amepongeza uwepo wa Kiwanda hicho na kusema kuwa, familia yake kwasasa imeondokana na ugonjwa huo baada ya kutumia kikamilifu dawa ya kuulia viluilui vya mbu.

Amesema hali katika familia yake inebadilika na hakuna tena mtu anayeugua malaria kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa tofauti na ilivyokuwa awali ambapo  wanafamilia walikuwa wakiugua malaria mara tatu hadi nne kwa mwezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...